Watoto wa kituo Cha Drive Change Foundation wakipata chakula
Mkurugenzi wa Taasisi ya Drive Change Foundation Peter Valentaine Masawe akiwa na watoto wanaolelewa katika kituo hicho.
Watoto wa kituo Cha Drive Change Foundation wakipata chakula cha mchana
Baadhi ya wazazi wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Drive Change Foundation wakiwa katika kikao cha kuchagua viongozi wa bodi wa shule hiyo ya awali.
Adedia Sumari mwenyekiti wa kitongoji cha Msongoro kijiji cha Ambureni kata ya Ambureni wilaya ya Meru mkoani Arusha akizungumza katika kikao cha kuchangua viongozi wa bodi wa shule kituoni hapo.
Wakwanza kushoto ni Mary Reuben Mwasa mshauei wa jamii walio katika mapambano ya AIDS Tanzania (WAMATA)
Baadhi ya Wazazi na walezi wawatoto wanalelewa katika kituo cha Drive Change Foundation wakiwa katika kikao cha kuchagua viongozi wa Bodi ya shule ya awali iliyopo kituoni hapo.
Baadhi ya Wazazi na walezi wawatoto wanalelewa katika kituo cha Drive Change Foundation wakiwa katika kikao cha kuchagua viongozi wa Bodi ya shule ya awali iliyopo kituoni hapo.
Na.Vero Ignatus,Meru.
Wito umetolewa kwa jamii kuwasaidia na kuwatunza watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi na siyo kujiachia serikali peke take kwani watoto hao ndiyo Taifa la kesho.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Drive Change Foundation Peter Valentaine Masawe kwamba watoto hao wanahitaji kuonyesha Upendo na malezi kwani watoto hao wanahitaji uangalizi mkubwa Ili na wao waweze kutimiza ndoto zao Kama walivyo watoto ambao hawapo katika mazingira hayo.
Masawe ambaye anamiliki kituo cha malezi ya watotoambapo ndani yake kuna shule ya awali iitwayo Drive change Foundation yenye jumla ya watoto 32 wakiume 15 wakike 17 amesema changoto kubwa anayokumbana nayo kwa watoto hao ni kuwabadilisha kutoka katika mguno walikuwa wanaoishi nao wa mtaaani Ili waweze kuwa katika mazingira ya kawaida
“Kazi hiyo ni ngumu Sana kwani watoto hao wanakuwa wametoka katika mazingira ambayo yalikuwa hayana uangalizi,wengine wanamadhaifu yao,uhakikishe unapambana kurudisha nidhamu,kwakweli yahitaji moyo Sana sivyo unaweza kukata tamaa kabisa”.alisema Peter
Amesema kuwa changamoto nyingine ni baadhi ya Walezi au wazazi hata baada ya kuwachukua watoto hao na kuwaingiza shuleni bado hawaoni umuhimu wa kuwajali tena watoto wao badala yake waneona ni jukumu la kituo wao wamejitoa
Peter alisema kuwa Amesema kwamba kituo kipo katika hatua za mwisho za kuwakatia bima ya Afya watoto hao wote 32 pamoja na kuwatafutia wafadhili katika masoko yao ikiwezekana kuanzia Elimu yao ya awali na kuendelea
Hadi Sasa wameshaweza kuwapatia watoto sita Ila (5) Kati yao wamepatiwa ufadhili wa Elimu ya shule ya Msingi kwa kuanza darasa la kwanza na mmoja kutokana na umri wake ulikuwa umezidi alipelekwa Ufundi wa magari Hadi Sasa anaendelea vyema
Aidha ndugu pita amewaomba wadau wowote kwa uaonde wa Elimu pamoja na wasamaria wema wajitokeze kwaajili ya kuwashika mkono katika kuhakikisha wanakamilisha majengo ya madarasa ya watoto pamoja na madawati kwani ujenzi umeshaanza wa madarasa sita na kuishia kwenye lenta na wameshindwa kupaua
“Hitaji letu ni mbao,Sementi,mbao za kupaulia,mialango
mabati,madirisha,mipango na mengine mengi. Kwa yeyote aliyepo tayari awasilane nasi kwa namba +255753630747
Matarajio yao ya baadae ni kuwa na kituo kilichokamilika kwaajili ya mahitaji ya watoto na kuifikia jamii kwa ujumla tukishirikiana na wadau mbalimbali,Sekta binafsi na Serikali kwa ujumla.
Mwisho.