Na
Mapuli Misalaba, Shinyanga
Jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea na uchunguzi wa tukio la kijana
anayefahamika kwa jina la Kulwa Sosoma
mwenye umri wa miaka 42 mkazi wa Ibinzamata katika manispaa ya Shinyanga ambaye
aliuawa kwa kushambuliwa na watu waliojichukulia sheria mkononi.
Hayo
yamebainishwa na kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna wa
Polisi Janeth Magomi ambapo amesema tukio hilo limetokea Octoba 24 katika kijiji cha Bugayambelele
baada ya kushambuliwa na watu waliojichukulia sheria mkononi wakimtuhumu
kuhusika na tuhuma za wizi.
Mjomba
wa Marehemu huyo Bwana Hamis Mathias ameelezea kuwa chanzo cha kifo cha kijana wao kimetokana na
kushambuliwa na watu wenye hasira kali ambao walimtuhumu kuhusika na tuhuma za
kuiba mpira wa maji unaotumika kumwagilia Bustani
Aidha jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga
limesema bado linaendelea na uchunguzi wa tukio la Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Tungu Sabuni Tungu
mwenye umri wa Miaka 60 mkazi wa kata ya usule Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga ambaye alifariki Dunia baada ya kukatwa panga na Bwana Nkwabi Joseph
mkazi wa kijiji hicho.
Tukio hilo limetokeo Oktoba 25,2023
majira ya saa tatu asubuhi kamanda wa Jeshi la Polisi
Mkoa wa Shinyanga kamishina wa polisi Janeth Magomi amethibitisha kuwa na taarifa za tukio
hilo,ambapo amesema Uchunguzi unaendelea ili kubaini waliohusika na mauaji
hayo.
Kamanda Magomi ametumia nafasi hiyo kuwaomba
wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na jeshi hilo ikiwemo
kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu unaojitokeza ili hatua za kisheria
zichukuliwe.