Na Mwandishi Wetu, APC BLOG, ARUSHA
Halmashauri ya Jiji la Arusha imetia saini mkataba mdogo (Addendum) na kampuni ya SINOHYDRO CONSTRUCTION LTD kutoka China ikiwa ni kazi ya nyongeza ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass inayotokea Olasiti yenye urefu wa kilomita 3.442 itakayo gharimu fedha za kitanzania bilioni 4.1
Ujenzi huu wa barabara ya Kisongo upo chini ya mradi wa TANZANIA STRATEGIC CITIES PROJECT (TSCP)-AF2 ambapo unahitajika kukamilika ndani ya miezi minne ikiwa ni kuanzia 11 Septemba 2019 hadi 11 Januari 2020.
Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mkataba huo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleimani Madeni akiambatana na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro Bukhay alisisitiza mkandarasi afanye kazi kwa ubora na kwa muda uliopangwa ili mradi huo ukawe faida kwa wananchi wa maeneo hayo.
Pichani: Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro Bukhay akisaini mkataba mdogo(Addendum) ya ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass
Pichani: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleimani Madeni akisaini mkataba mdogo(Addendum) ya ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass