Jumuiya ya wazazi ccm wilaya ya shinyanga mjini yakemea wanaume wanaotelekeza familia

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

TAZAMA HII VIDEO

Jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini
imekemea suala la wanaume kutelekeza familia zao na kwamba linasababisha
mmomonyoko wa maadili pamoja na ukatili kwa watoto katika jamii na Taifa kwa
ujumla.

Hayo yamesungumzwa katika ziara ya kamati ya
utekelezaji jumuiya ya wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya
Shinyanga mjini wakati ikitembelea miradi ya maendeleo na kukagua  uhai wa jumuiya kata ya Kizumbi na kata ya
Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya
Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko pamoja na mambo mengine amekemea suala hilo
huku akitaja athari zake ambapo pia ameiomba serikali kuchukua hatua kwa mzazi
anayebainika kutelekeza familia na kwamba hali hiyo itasaidia kuimarisha
familia.

“Baba
anapomtelekeza mke na watoto, watoto wale nani atawatunza jambo hili kama wazazi
tunalikemea mchezo huu wa Baba kutelekeza familia siyo jambo nzuri tunatakiwa
tuwe na msaada mkubwa kwa wanaotendewa unyanyasaji huu, huyo Baba anatakiwa
atafutwe akamatwe arudishwe mpaka nyumbani kwake lakini serikali inatakiwa
kumchukulia hatua za kisheria”.

“Athari
ya kwanza wanawake wengi wanakosa uwezo wa kuwasomesha watoto baada ya
kuathirika kiuchumi utakuta watoto hawasomo hata kama watasoma lakini mavazi
wanayovaa mara nyingi siyo ya heshima lakini ukweli ni kwamba suala hili
ninawaathiri sana watoto na kusamabisha watoto kwenda mitaani kwa sababu wanakosa
malezi bora ya wazazi wawili Baba na Mama”.
amesema mwenyekiti
Mrindoko

Kwa upande wake katibu wa jumuiya ya wazazi CCM Wilaya
ya Shinyanga mjini Bi. Doris Kibabi naye amekemea tabia za wanaume kukataa
mimba baada ya kumbebesha ujauzito mwanamke ambapo amesema hali hiyo
inawaathiri kisaikolojia wanawake na kupelekea ugumu wa maisha yao ya kila
siku.

“Wapo
baadhi ya wanaume wanatabia za kuwapa mimba wanawake halafu wanazikataa, mwanamke
anabeba mimba miezi 9 mpaka anazaa akizaa analea huyo mtoto mpaka anakua mtoto
akipata mafanikio Baba anajitokeza ndiyo maana unakuta watoto wengine siku hizi
wanawakana wazazi, wewe unasifa gani ya kuwa Baba wakati ulimpa mimba mwanamke
ukamkataa jiulize hivi angeitoa hiyo mimba ungejitokeza”.

“Niwaomba
wanawake msikate tamaa mwanaume akikataa mimba wewe toa taarifa kwa viongozi
husika halafu endelea kuilinda ukijifungua mlee mtoto bila malalamiko Mungu
atakusaidia”.
Amesema katibu wazazi Bi. Doris Kibabi

Baadhi ya wazazi nao wamekemea suala hilo huku
wakiipongeza kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga
mjini kwa kufanya ziara hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu katika masuala
mbalimbali ikiwemo ukatili, utunzaji wa mazingira pamoja na uimarishaji wa
jumuiya hiyo.

Kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya
Shinyanga mjini imeendelea na ziara kutembelea miradi mbalimbali ya maendelo
pamoja na kukagua uhai wa jumuiya za wazazi kwenye kata ambapo leo Jumanne Mei
16,2023 imetembelea kata ya Kizumbi na kata ya Ibinzamata.

Wajumbe mbalimbali wa kamati hiyo wametoa elimu katika
masuala mbalimbali ikiwemo kupinga vitendo vya ukatili, kuimarisha malezi ya
watoto kwenye familia,  elimu na haki za
watoto na afya huku wakisisitiza ushirikiano ili kuimarisha jumuiya ya wazazi
CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.

 

 

Kamati ya utekelezaji CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo
Mei 16,2023 ikiendelea na ziara kwenda kukagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha
Bugayambelele kata ya Kisumbi Manispaa ya Shinyanga.