Kamati ya pic yaitaka benki ya nmb kuangalia uwezekano wa kuongeza gawio kwa serikali

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Kamati
ya  kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa mitaji ya umma [PIC] imeitaka benki
ya NMB kuangalia uwezekano wa kuongeza gawio kwa serikali hali
itakayosaidia  kuongeza mapato katika kuchangia mfuko mkuu wa Serikali.


Akizungumza
bungeni jijini Dodoma Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya
Uwekezaji wa mitaji ya umma [PIC] Dkt Raphael Chengeni amesema hatua
hiyo itafanikisha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo
hapa nchini.

Katika
hatua nyingine Dkt Chengeni amemuagiza mwenyekiti wa bodi ya benki  ya
NMB  Profesa Joseph Semboja kuhakikisha anapeleka mbele ya kamati hiyo
mchakato mzima  wa kumpata mtendaji mkuu wa benki hiyo ili kutoa fursa
kwa watanzania wenye uwezo na weledi wa kuongoza taasisi kubwa za
kifedha wanajitokeza kwa ajili  ya maslahi mapana ya taifa .

Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Bi Ruth Zaipuna amesema benki yake
inaunga mkono miradi mikubwa ya kimkakati ya serikali ikiwemo ujenzi wa
reli ya kisasa (SGR) ili kurahisisha shughuli mbalimbali za kimaendeleo
kwa mwananchi mmoja mmoja  .

Kamati 
mbalimbali za bunge zinaendelea na vikao vyake jijini dodoma tangu
Januari 13,2020 huku kikao cha 18 cha Bunge  kikitarajia kuanza Januari
,28,2020.