Kampuni ya nyanza yapigwa marufuku dar

Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda ametaka umakini katika utoaji
wa tenda za ujenzi wa miradi mbalimbali ili kuepuka dosari.

Makonda ameyasema hayo leo, Jumamosi, Novemba 2, 2019, wakati akiwa
kwenye ziara ya kukagua miradi ya kimkakati inayoendelea katika wilaya
za Ilala na Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Aidha, Makonda ametoa agizo kuwa Kampuni ya Nyanza inayosimamia mradi wa
ujenzi wa Daraja la Mto Kivule isipewe tenda yoyote baada ya
kukamilisha mradi huo, kutokana na kushindwa kukamilisha baadhi ya
miradi ambayo wamewahi kupewa. Hata hivyo, Mkandarasi huyo tayari,
ameanza ujenzi wa mradi huo baada ya kusikia RC Makonda anakwenda huko.


“Huyu
mkandarasi huu uwe mradi wake wa mwisho katika Jiji la Dar es Salaam.
Kama mnakumbuka hata Temeke aliwahi kufanya uzembe wa namna hii, vifaa
hana vya kutosha kazi yenyewe haieleweki, tunataka Makandarasi wenye
kasi kutekeleza miradi ya maendeleo,” amesem Makonda.

Amesema baadhi ya Makandarasi wanapewa tenda na kuishia kulipa madeni
yanayowakabili kutokana na fedha wanazoingiziwa kukatwa na kusababisha
miradi kutokamilika kwa wakati.
“Mnapotoa hizi tenda mjiridhishe wengine ndio kama hawa ambao hadi leo
kazi hazionekani,  pia msiwape kazi kwa rushwa mtashindwa kusimamia
miradi hii muhimu kwa wananchi,” amesema Makonda


Hivi
karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, alitoa agizo
la kuwekwa rumande kwa mkandarasi huyo kutokana na kusuasua kwa ujenzi
huo.

Kwa upande mwingine, Mkandarasi anayejenga Machinjio ya Kisasa ya
Vingunguti, Elisante Ulomi amesema, mradi wa machinjio ukikamilika
utaongeza pato la Taifa kwa kuwa kila kitu kitakachoptoakana na zao la
mifugo kitauzwa kwa mfano pembe, damu, ngozi, kwato na nyama ambapo
Serikali itakusanya mapato na wananchi watafanya biashara kirahisi
katika mazingira rafiki.
Katika hatua nyingine Makonda amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) kutokana na kasi ya utekelezaji wa mradi wa Machinjio ya kisasa
katika eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam.