Ubalozi wa marekani nchini iraq washambuliwa tena

Marekani
imeitolea mwito Iraq kulinda majengo yake ya kidiplomasia baada ya
ubalozi wake mjini Baghdad kushambuliwa kwa maroketi matatu. 


Msemaji
wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani ametoa mwito kwenye taarifa
yake kwa Iraq kutimiza wajibu wake wa kuyalinda majengo hayo. 

Jana
Jumapili roketi moja lilishambulia eneo la kulia chakula kwenye ubalozi
wa Marekani nyakati za chakula cha jioni, wakati maroketi mengine
mawili yakiangukia karibu na eneo hilo, hii ikiwa ni kulingana na chanzo
kilichozungumza na shirika la habari la AFP. 

Amesema
tangu Septemba mwaka jana kumekuwepo na mashambulizi 14 yanayofanywa na
wanamgambo wa Iran na wanaoungwa mkono na Iran dhidi ya watumishi wa
Marekani waliopo Iraq. 

Amesema, hali ya usalama ni ya wasiwasi na makundi yenye silaha yanayoungwa mkono na Iran yanaendelea kusalia kitisho.