Katibu mkuu ccm : hatima ya makatibu wakuu wastaafu adbulrahman kinana , yusuph makamba na benard membe itajulikana wiki hii

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

RIPOTI
kuhusu tuhuma zinazowakabili makatibu wakuu wastaafu wawili(Adbulrahman
Kinana na Yusuph Makamba) akiwemo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje,
Bernard Membe tayari imekamilika na inatarajiwa kukabidhiwa kwa Kamati
kuu ya Chama cha Mapinduzi mwishoni mwa wiki hii na kamati ndogo ya
nidhamu chini ya uongozi wa Makamu Mwenyekiti wa chama, Bara Philip
Mangula.


Kauli
hiyo ilitolewa jijini hapa jana na Katibu Mkuu wa chama, Dk Bashiru
Ally wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala matatu
yakiwemo kuanza kwa vikao vya kamati kuu ya chama mwishoni mwa wiki,
ziara ya siku tatu mkoani Mtwara na ugeni wa wanachama wapya kujiunga
CCM.

Dk.
Bashiru alisema kuwa siku saba zilizotolewa na kamati kuu ya chama
zimeshamalizika ambapo taarifa hiyo itapitiwa kesho kutwa na kamati
ndogo ya nidhamu ya chama ili iwasilishwe kwa kamati kuu mwishoni mwa
wiki.

“Kamati
kuu itakaa mwishoni mwa wiki hii ili kupokea taarifa ya Mangula hivyo
wiki hii wakati vikao vikianza kamati hizo mbili kuu na ndogo ya nidhamu
na maadili zitakaa,”alisema Dk. Bashiru.

Alifafanua
kuwa uamuzi wa  chama ni kuwa taarifa ya Mangula ipo tayari kwa ajili
ya kuwasilishwa kwenye vikao vya chama ambapo baada ya vikao Polepole
atatangaza kama wamebainika kuwa na makosa na hatua gani zitachukuliwa
na kwa adhabu gani.

Alisema
yapo makossa mengine ukithibitika adhabu yake haitangazwi na baadala
yake anaambiwa mhusika na kwamba saa nyingine inaweza ikatolewa adhabu
ya onyo kali hiyo itatangazwa hadharani.Pia unaweza kukosa aina fulani
ya haki zako za uanachama .

“Ukithibitika
umefanya makosa ya kukiuka kanuni hiyo mtu mwingine anakosa haki za
uanachama na kuwa chini ya uangalizi.. lakini wakati mwingine mtu
anapewa karipio kuliko onyo kali kama utaratibu wa kulitumikia ana muda
wa uangalizi ili ajirekebishe,”

Alifafanua
wakati mwingine hupelekea mhusika kuachishwa uanachama na kuwa raia
huru lakini anaweza kujiunga tena na kujiunga kwa mujibu wa taratibu za
kikanuni na kama ni kiongozi anaweza kusimamishwa uongozi kwa muda au
kuachishwa.

Alifafanua
kuwa adhabu hizo hutolewa baada ya watuhumiwa kusikilizwa, kujitetetea
na baada ya kamati kuu kuchambua na kujiridhisha ili kutoa uamuamuzi.

“Kwa
hiyo kuhusu hatua zitakazochukuliwa ni baada ya vikao vya kamati kukaa
na kupokea taarifa ndio uamuzi utatolewa, hivyo taarifa ya Mzee Mangula
itawasilishwa ndani ya kamati kuu mwisho wa wiki hii,”alisema.

Aidha,
Dk. Bashiru amekanusha taarifa zilizosambazwa mtandaoni na baadhi ya
watu kuhusu ziara yake mkoani Mtwara kuwa alikuwa akilindwa na askari
polisi si za kweli.

“Kuna
watu wameshaharibu sifa ya ziara yangu wametengeneza picha inayoonyesha
gari la rangi ya kijani wanayoiita ya katibu mkuu halafu imezungukwa na
polisi akaandika umoja wa vijana wakimlinda katibu mkuu wa CCM.

“Zipo
mamlaka zinazoweza kusimamia matumizi bora ya mtandao nakanusha maana
ziara yangu ilifanyika mchana na waandishi wa habari ni mashahidi hivyo
tusaidiane kueleza kama ni kweli tulilindwa na viongozi wa
dola,”alisema.

Aliongeza:
“sio ziara yangu ya kwanza kufanyika mara nyingi huwa Napata ulinzi wa
askari wa barabarani ni wa kawaida sina sababu ya kulindwa maana vyombo
hivyo vinafanya kazi kwa mujibu wa sheria.

“Wana
CCM tutumie vizuri mitandao ya kijamii nimemwelekeza Polepole aeleze
sio gari la Katibu Mkuu na ziara ya Mtwara haikuwa hivyo na vyombo
husika chukueni hatua.”