Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwa ziara ya kikazi kusikiliza kero za wakulima wa chai, kulia ni mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Brigedia jenerali Marko Gaguti.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akikagua moja ya shamba la chai, katika eneo la Maruku mkoani Kagera.
Muonekano wa nje wa kiwanda cha Kagera Tea Company kinachojihusisha na uchakataji wa chai.
Moja ya shamba la chai lililoko Maruku mkoani Kagera.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akizungumza na wakulima, menejimenti ya kiwanda na wafanyakazi wa kiwanda cha Kagera tea company.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akikagua mashamba ya chai Mkoani Kagera huku akisikiliza kero mbalimbali kutoka kwa wakulima.
…………………………………………………..
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, amefanya ziara katika kiwanda cha chai cha Kagera Tea Company kilichopoeneo la Maruku mkoani humo. Kabla ya kuanza ziara hiyo, Mhe. Waziri alikutana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Brigedia Jenerali Marko Gaguti ambapo alipata taarifa fupi kuhusiana nahali ya Viwanda vya chai Mkoani Kagera.
Mhe. Waziri amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti kwa juhudi anazozifanya katika kuchochea maendeleo ya Viwanda na ukuzaji wa uchumi mkoani Kagera.
Mhe. Waziri Bashungwa alieleza lengo la ziara ni kuwatembelea wakulima wa chai katika mkoa huo na kukutana na mwekezaji wa kiwanda cha Kagera Tea Company kilichopo eneo la Maruku ambacho kimekua kikisuasua katika uzalishaji.
Akiwa kiwandani hapo Mhe. Bashungwa alikutana na wakulima wa chai ambao ndio wazalishaji wakubwa wamalighafi katika kiwanda hicho. Mkulima Philemon Stambuli alieleza kuwa kilimo kimeshuka kwa asilimia 80 na wakulima wamekata tamaa kutokana na changamoto mbalimbali zinazosababishwa na kiwanda hicho.
Alizitaja changamoto hizo ni wakulima kufanya kazi na kiwanda bila mikataba ya kazi, ambapo inapunguza kipato cha mkulima na uhakika waajira. Nyingine ni kucheleweshewa malipo na mmiliki wa kiwanda ambayeni mzawa, Miezi mitatu sasa imepita, wakulima wanadai zaidi ya milioni 40 kinyume na makubaliano ya kulipwa tarehe 15 ya kila mwezi.
Bwana Stambuli ameeleza changamoto nyingineni kwa muwekezaji wa kiwanda kuchelewa kuchukua chai baada ya kuvunwa hivyo kupelekea chai kupoteza ubora wake.
Naye ndugu Nyantaba Yahya Hassan, mkulimawa chai ameeleza changamoto ya kukosa ushirikiano kutoka kwa baadhi watendaji wa Serikali Ofisi ya Wilaya kama afisa kilimo pamoja na wakala wa wakulima wadogo wa chai Tanzania pamoja na taasisi nyingine ambazo zinazohusika katika uendelezwaji wa zao la chai.
Kwa upande wake, mmiliki wa kiwanda hicho amekuwa akilalamikia wakulima wasio waaminifu ambapo wanamuibia na kupeleka kilo chini ya makubaliano.
Baada ya kusikiliza kero kutoka kwa wakulima aliitisha kikao kati ya wakulima na msimamizi wa kiwanda cha Kagera Tea Company ilikujadili kwa pamoja changamo tozo tena kusikiliza pande zote mbili ili kutoa maamuzi ya pamoja.
Msimamizi wa kiwanda hichoalikirikutolipadeni la wakulima ambalo ni zaidi ya milioni 40, malikimbikizo ya mishahara na madeni ya wafanyakazi kiasi cha shilingi milioni 108,
Mhe. Bashungwa alisikitishwa kwa kupuuzwa kwa maagizo yake aliyoyatoa kwa bodi ya chai tarehe 16 Januari, 2019 akiwa naibu waziri wizara ya kilimo kwamba bodi ikae na wakulima pamoja na muwekezaji na kutatua changamoto zote za wakulima lakini hadi amerudi tena kuwatembelea wakulima hao wa chai tarehe 19 Desemba, 2019 bado anakuta changamoto ni zilezile na maagizo ya Serikali hayajafanyiwa kazi.
Mhe. Bashungwa amewahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, imedhamiria kuinua zao la chai kwa kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo chao, pia kuhakikisha wakulima wanapata stahiki zao na kwa wakati.
Ameendelea kusema kuwa Serikali itahakikisha minada ya chai inafanyika ndani ya nchi ili kuwasaidia wakulima na kupanua soko la ndani.
Aidha, Mhe. Bashungwa alitoa maagizo kwa mwenye kiwanda kulipa madeni ya wakulima na wafanyakazi kabla mwaka huu haujaisha ifikapo tarehe 31 Desemba, 2019. Mhe. Bashungwa aliahidi kurudi tena kiwandani hapo mapema Januari kuhakikisha kama wakulima wamelipwa.
Nao wakulima wa chai wa mkoa wa Kagera wamemshukuru Rais Mhe. Magufuli kwa kumteua Mhe. Bashungwa kama Waziri wa Viwanda na Biashara kwani amekuwa akiwafuatilia mara kwa mara kutatua kero zao.