Kufanya sana mapenzi kunapunguza siku za kuishi….babu wa miaka 85 atoa ushauri

Manju Mstaafu James Makungu Sombi

Imeelezwa kuwa unywaji pombe,kufanya
sana mapenzi na ulaji mbaya unachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza siku
za kuishi kwa binadamu.



Hayo yamesemwa na Mzee James Makungu Sombi aliyezaliwa mwaka 1934 katika
kijiji cha Mwamanga wilayani Magu mkoani Mwanza wakati akizungumza na
Malunde 1 blog leo Jumapili Oktoba 27,2019 nyumbani kwake Kisesa jijini
Mwanza.
Mzee Sombi ambaye sasa ana umri wa miaka 85 na bado nguvu za kutosha
anasema siri pekee ni kwamba aliepuka matumizi ya pombe,kuepuka kufanya
sana mapenzi na kula vyakula vya asili.
“Vyakula vya asili vinajenga mwili vizuri kuliko hivi vyakula vya
kisasa mnavyokula,ukifanya sana mapenzi unaharibu mwili wako,walau fanya
mapenzi mara mbili au mara tatu kwa wiki hapo ndipo utajenga mwili wako
vizuri na epuka kunywa pombe kali zikiwemo gongo,hizi zinaharibu mwili”
,amesema Mzee Sombi.
“Ukiona umeanza kuzeeka unatakiwa uanze kufanya mazoezi mbalimbali
ikiwemo kutembea ili kunyoosha misuli na utumie vyakula vya asili
ikiwemo ugali wa mtama,uji wa ulezi”
,ameongeza
Mzee Sombi ni miongoni mwa waanzilishi wa Makumbusho ya Kisukuma ya
Bujora yaliyopo Kisesa jijini Mwanza,ni Manju mstaafu aliyebahatika
kutembelea nchi mbalimbali za Ulaya akitangaza utamaduni wa Kisukuma
akiambatana na Padri David Clement ambaye alitoa wazo la kuanzishwa kwa
Makumbusho ya Bujora.
Mwaka 2005 Mzee Sombi alikaribishwa nchini Denmark kuonesha jinsi
Wasukuma walivyokuwa wanamuomba Mungu kwa njia za asili kabla ya kuingia
dini za kigeni.
Mzee Sombi ni Mtaalamu wa Masuala ya Utamaduni wa Kabila la Kisukuma,Wasiliana naye kwa namba  0755903972
Mwaka 2005 Mzee Sombi akitoa burudani ya Ngoma ya zeze nchini Denmark
Mwaka 2005 Mzee Sombi akitoa burudani nchini Denmark
Mzee Sombi akionesha namna Wasukuma walivyokuwa wanamuomba Mungu kabla ya kuja kwa dini za kigeni