Maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne na pili yaanza kagera.



Na Silvia Mchuruza, Bukoba

Kufuatia maandalizi
ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne na pili mwaka huu afisa elimu
sekondari wa manispaa ya Bukoba Mwl. Emmanuel Ebeneza amezungumzia zaidi
maandalizi ya mtihani huo  na kuwataja watahiniwa wanaotegemea kufanya
mtihiani huo.
 

Akizungumza na vyombo
vya habari ofisini kwake Mwl.Emmanueli amesema kuwa watahiniwa
wanaotegemea kufanya mtihani huo wamegawanyika makundi matatu kundi la
kwanza  ni wale walio shuleni, kundi la pili ni wale wanaojitegemea na
kundi la mwisho ni wale wanaorudia mtihani hili kukidhi vigezo vya
kufanya mtihani wa kidato cha nne.
 

Aidha ameongeza kuwa
jumla ya watainiwa wote kupitia makundi hayo ni 2847 ikiwa watainiwa
walio shule ni 2012 ambapo wasichana ni 1237 na wavulana ni 1080 pia na
wanarudia mitihani wavulana ni 217 na wasichana ni 240 pamoja na wale
wanaofanya mtihani huo hili kukidhi vigezo wavulana ni 36 na wasichana
37.
 

Pia amesema kuwa
mtihani huo wa kidato cha nne unategemea kufanyika tarehe 04/11 mpaka
tarehe 22/11 mwaka huu ikiwa manispa ya bukoba itakuwa navituo 30 kwa
watahiniwa walio shuleni na vituo 7 kwa wale wanaojitegemea.
 

Vilevile amewataja
watahiniwa wanaotarajia kufanya mtihani wa kidato cha pili katika
manispa ya Bukoba ni 2714 ikiwa wasichana ni 1476 na wavulana ni 1238
ambapo mtihani huo unatarajiwa kuanza tarehe 11/11 mpaka tarehe 22/11
mwaka huu.
 

Sambamba na hayo
amewaomba wanafunzi wa manispaa ya Bukoba mkoani humo kuhakikisha
wanajiandaa vyema kuelekea mitihani hiyo hili kuweza kufikia malengo yao
na kuwaomba wazazi kuwasisitiza bidii katika masomo ya watoto wao.