Mahakama ya iran yamhukumu kifo jasusi wa cia

Msemaji
wa Idara ya Mahakama nchini Iran Bw. Gholam Hossein Esmaili, amesema
Mahakama Kuu ya nchi hiyo imemhukumu kifo raia mmoja wa Iran ambaye ni
jasusi wa Shirika la Upelelezi la Marekani, CIA.


Shirika
la habari la Iran Fars limemnukuu Bw. Esmaili akisema kuwa, Amir
Rahimpour, ambaye alikuwa mpelelezi wa CIA, alipewa kiasi kikubwa cha
pesa ili kutoa baadhi ya taarifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran kwa
idara ya ujasusi ya Marekani.

Ameongeza
kuwa watu wengine wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 kila mmoja
gerezani kwa tuhuma za kufanya upelelezi kwa ajili ya Marekani.