Mh ummy aanza kazi rasmi,afanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara “mimi siyo mbunge wa ofisini

 
IMG-20201125-WA0098
MBUNGE
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akisaini kitabu cha wageni
mara baada ya kufika kwenye ofisi za Tarura wilaya ya Tanga wakati wa
ziara yake

IMG-20201125-WA0096
IMG-20201125-WA0091
MBUNGE
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akilakiwa meneja wa Tarura
wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene mara baada ya kufika kwenye
ofisi za Tarura wilaya ya Tanga wakati wa ziara yake
IMG-20201125-WA0097

IMG-20201125-WA0094
MBUNGE
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akisistiza jambo kwa Meneja
wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene kushoto wakati wa
ziara yake

IMG-20201125-WA0093MBUNGE
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akionyeshwa maeneo
mbalimbali kwenye mifereji wakati wa ziara yake na Meneja wa Tarura
wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene
IMG-20201125-WA0095MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akionyeshwa maeneo
mbalimbali kwenye mifereji wakati wa ziara yake na Meneja wa Tarura
wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene
IMG-20201125-WA0099MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wa pili kutoka kulia akitembelea  maeneo
mbalimbali wakati wa ziara yake wa kwanza kushoto ni Meneja wa Tarura
wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene

IMG-20201125-WA0092
MBUNGE
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wa pili kutoka kushoto
akionyeshwa maeneo mbalimbali kwenye mifereji wakati wa ziara yake na
Diwani wa Kata ya Msambweni (CCM) Godias Kimath na kwanza kulia Meneja
wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene
IMG-20201125-WA0090

MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Mh  Ummy Mwalimu ameanza kazi rasmi leo 
za jimbo kwa kutembelea ujenzi na kukagua miradi ya barabara, mifereji
na madaraja ya kata nne ambazo ni Mnyanjani, Mabawa, Msambweni na
Ngamiani kati za halmashauri ya Jiji la Tanga ambazo zitagharimu kiasi
cha sh.bilioni 2.9.

Ummy alisema kuwa ameanza kazi kwani Chama cha Mapinduzi (CCM) kiliahidi
na sasa  kinatekeleza Ilani ikiwemo matengenezo ya barabara ya karume
mpaka  machinjioni mita 600 ambayo itajengwa kwa kiwango cha changarawe,
barabara ya karume mpaka zahanati ya kwanjeka kwa kiwango cha
changarawe,
 
Huku akiitaja pia barabara ya 11 na 12 kuzunguka soko la Ngamiani  itawekwa
lami,barabara ya Mabawa mpaka Msambweni ambayo itaongezwa lami yenye
urefu wa kilometa 2.

Aidha pia amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia fedha Tarura ambazo
zitaenda kuboresha miundo mbinu ya barabara ndani ya Jimbo la Tanga
Mjini na kuwa kazi ndiyo zimeanza na hatakuwa mbunge wa ofisini bali
muda mwingi atakuwa ni wa kutembelea miradi na kutatua kero za wananchi
wa Tanga.

Naye Meneja wa
Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene amesema kuwa  kwa
mwaka huu wa fedha wamesaini mikataba mitano  ambapo ndani ya siku 14
wataanza kazi utekelezaji .
 
Miradi hiyo ipo
itayayotekelezwa kwa kiwango cha changarawe, lami ,ujenzi madaraja na
ukarabati wa mifereji  ndani ya Jiji la Tanga barabara na amesema kuwa
watendelea kufanya kazi kama azma ya serikali ya hapa kazi tu.

kwa
upande wa madiwani  akiwemo Yakub Nuru ambaye  Diwani wa Mnyanjani wametoa
shukrani kwa mh. Ummy Mwalimu pamoja na serikali kupitia Rais Magufuli 
kwa kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya barabara. 
 
Awali naye Diwani
wa Kata ya Mabawa, Athumani Babu alisema kuwa ilani ya chama cha
mapinduzi imeanza kutekelezwa  kwani barabara ya kutoka komesho mpaka 
chai bora yenye km 1   imeweka lami .
Hata hivyo kwa upande wake Diwani
wa kata ya Ngamiani Kati, Habibu Mpa ametoa shukrani zake kwa mh.
mbunge ummy mwalimu kwa  kufuatilia ahadi ya waziri mkuu wakati
akifungua kampeni  za Mbunge kuhusu kuweka lami barabara ya 11 na 12
yenye urefu wa mita 600.