Mvua yaua watu 14 tanga




Na Rajabu Athumani, Mwananchi 


Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Tanga
zimezidi kusababisha maafa baada ya vifo vingine vitatu kuripotiwa na
kufanya idadi ya waliokufa kufikia 14 hadi leo Jumapili Oktoba 27, 2019
saa 5 asubuhi.




Polisi wamethibitisha kupatikana mwili
mmoja katika kitongoji cha bwawani kata ya Sindeni, na miili ya watoto
wawili iliyokutwa mtaa wa Wandama kata ya Kwenjugo wilayani Handeni.




Jana mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin
Gondwe alisema watu 10 wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kutumbukia kwenye maji kutokana na barabara kukatika,
mwingine kusombwa na maji.




Akizungumza leo mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya Handeni, William Makufwe amesema miili iliyopatikana ni mitatu.




Joan Luvena, ofisa habari wa Jeshi la
Uokoaji na Zimamoto wilayani Handeni amesema juzi watu 51 walilala juu
ya mti katika mtaa wa Kwamaraha kutokana na makazi yao kuzingirwa na
maji.




Miili hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Handeni.


Chanzo – MWANANCHI