Naibu waziri mabula ataka majina ya watumishi wa ardhi waliokacha kwenda mafia


Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Mafia mkoani Pwani Shaib Nnunduma
baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mafia jana kuanza ziara ya
siku mbili wilayani humo. Katikati ni Mbunge wa jimbo la Mafia Mbaraka
Dau.



Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akisalimiana na uongozi wa wilaya ya Mafia mkoani Pwani baada ya
kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mafia jana kuanza ziara ya siku mbili
wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma.



Mbunge
wa jimbo la Mafia Mbaraka Dau akisisitiza jambo mbele ya Naibu Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula katika ofisi
ya Mkuu wa wilaya ya Mafia wakati Naibu Waziri alipoanza ziara yake ya
siku mbili wilayani Mafia mkoani Pwani. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Mafia Shaib Nnenduma.


……………………

Na Munir Shemweta, MAFIA

 

Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
ameagiza kupatiwa majina ya watumishi saba wa sekta ya ardhi
awaliopangiwa kuhamia halmashauri ya wilaya ya Mafia mkoani Pwani lakini
wameshindwa kuripoti katika kituo chao kipya cha kazi.


Dkt
Mabula alitoa agizo hilo jana mwamzoni mwa ziara yake ya siku mbili
katika wilaya ya Mafia mkoani Pwani kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya
serikali kupitia kodi ya ardhi, kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya
ardhi kwa njia ya kielektroniki, kukagua Masijala ya ardhi pamoja na
kutatua migogoro ya ardhi.


Kauli
ya Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inafuatia
kuelezwa na Mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma kuwa wilaya yake ina
mtumishi mmoja wa sekta ya ardhi jambo linaloifanya wilaya hiyo
kushindwa kutekeleza majukumu ya sekta hiyo ipasavyo.


Dkt
Mabula alisema, Wizara yake italifanyia kazi suala hilo mapema kwa kuwa
ni vigumu wilaya kufanya kazi vizuri katika sekta ya ardhi kwa kutegemea
mtumishi mmoja hasa ikizingatiwa sekta hiyo inahitaji kuwa na wapimaji,
wathamini pamoja na wataalamu wa mipango miji.


‘’Mafia
mna mtumishi mmoja wa sekta ya ardhi? Suala hili inabidi lifanyiwe kazi
mapema na wizara yangu italifanyia kazi kuhakikisha wilaya inakuwa na
watumishi wa njanja zote katika sekta ya ardhi’’ alisema Dkt Mabula


Awali
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma alimueleza Naibu Waziri Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa, changamoto kubwa
inayoikabili wilaya yake kwa upande wa sekta ya ardhi ni kukosekana
watumishi wa kutosha ambapo wilaya hiyo imekuwa na mtumishi mmoja wa
sekta hiyo kwa muda mrefu baada ya mtumishi mmoja wa Uthamini kupangiwa
majukumu mengine.


Kwa
mujibu wa Nnunduma, jitihada za wilaya yake kufuatilia upatikanaji
Watumishi wa sekta ya ardhi zimeonekana kukwama kwa kuwa hadi sasa
hawajapata mtumishi mwingine jambo linaloifanya wilaya hiyo kushindwa
kutekeleza vyema majukumu ya sekta hiyo.


‘’Watumishi
saba walipangiwa kuja Mafia lakini wameshindwa kuripoti na hapa
unavyotuona tuna mtumishi mmoja, hatuna wataalamu kama wangekuwepo
wangesaidia upangaji. Wilaya ni kama imesimama katika sekta ya ardhi’’
alisema Nnunduma 


Nnunduma
alisema, ujio wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
inaweza kuwa faraja kwao kupata watumishi kwa kuwa tangu kuteuliwa kwake
na Rais John Pombe Magufuli kuongoza wilaya ya Mafia ndiyo anashuhudia
Waziri wa kwanza wa sekta ya ardhi kwenda wilaya hiyo aliyoieleza kuwa
kama itatumiwa vizuri basi itaiwezesha serikali kuingiza mapato mengi
kupitia sekta ya utalii.


Mbunge
wa jimbo la Mafia Mbaraka Dau alimueleza Dkt Mabula kuwa, pamoja na
changamoto nyingine lakini Wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la
ukosefu wa la Baraza la Ardhi la nyumba
  la
wilaya jambo linalowalazimu wananchi kufunga safari hadi katika Baraza
la Mkuranga kitu alichokieleza kinawafanya baadhi ya wananchi kushindwa
kwenda na hivyo kupoteza haki zao.