Naibu waziri wa maji amfuta kazi mkandarasi wa kampuni ya eker njombe baada ya kubaini hana uwezo

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso


 
Na Mwandishi Wetu Njombe

Naibu waziri wa maji Juma Aweso amemfuta kazi mkandarasi wa
kampuni ya Eker.co.ltd aliekuwa akitekeleza mradi wa maji wa Lifua-Manda
wilayani Ludewa mkoani Njombe wenye thamani ya zaidi ya mil 585
wilayani Ludewa mkoani Njombe kwa madai ya kuto ridhishwa na uwezo wake.


Kampuni hiyo ilingia mkataba wa maboresho ya mfumo wa mabomba
2017 na kutakiwa kukabidhiwa serikalini 2018 jambo ambalo limeshindwa
kutekelezeka hadi sasa na kusababisha kilio kikubwa kwa wananchi ambao
wanai tangu huduma ya maji ikosekane kijijini kwao 2009 maradhi ya tumbo
hayaishi.


Akizngumza mara baada ya kusikiliza kilio cha muda mrefu cha
wakazi wa kijiji cha Lihagule ambacho ni miongoni mwa vijiji vinne
vilivyokuwa vikinufaika na mradi huo kabla miundombinu yake kuchoka na
kuilazimu serikali kuona umuhimu wa maboresho ,naibu waziri wa maji Juma
Aweso anasema serikali imejiridhisha kuwa mkandarasi huyo hana uwezo
kwa kuwa kazi iliyokuwa ikamilike baada ya miezi minne ameshindwa
kuifanya katika kipindi cha miaka minne na kuagiza halmashauri
kutekeleza kupitia mafundi wa ndani.


Baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo akiwemo Rejina Matei,Atu
Mtweve na Laurent Muhagama wanasema kukosekana kwa huduma ya maji ya
bomba kijiji kwao kumesababisha akina mama kuliwa na mamba kutokana na
kufata maji katika mto ruhuu huku wengine wakidai ndoa nyingi
zimevunjika kwasababu ya kutumia muda mwingi kufata maji mabondeni.


Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya ludewa Adrea tsere
anatumia fursa ya mkutano huo wa naibu waziri wa maji kutoa onyo kwa
mwananchi ambaye hatajiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ambapo
amesema yeyote ambaye hatafanya hivyo anawekwa rock up huku akiwataka
wenyeviti wa vijiji kumpa taarifa ya waliosusia.