Nchi za sadc zasuasua kuridhia itifaki ya mazingira

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Malisili na Utalii ,Prof ,Adolf Mkenda akizungumza
wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu wakuu na Maafisa Waandamizi wa
Sekta za Mazingira ,Malisili na Utalii kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ,
kusini mwa Afrika (SADC) .


 

Na Claud Gwandu,Arusha
PAMOJA na athari za mabadiliko ya tabianchi kuzikumba
nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa  Afrika(SADC),nchi hizo bado zinasuasua
kuridhia itifaki ya utunzaji wa mazingira, miaka mitano tangu ilipopitishwa.
 Itifaki hiyo pamoja na mambo meingine,ina malengo ya
kuhifadhi mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu na ilipitishwa mwaka 2014
na Kikao cha wakuu wa nchi  wa Jumuiya
hiyo yenye wanachama nchi 16.
 Hadi sasa ni nchi tatu tu kati ya 16 zilizoridhia
itifaki hiyo ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini,Msumbiji na Zambia huku Tanzania
ikielezwa kuwa katika hatua za mwisho za mchakato wa kuridhia itifaki hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu  wa Rais(Mazingira),Joseph Malongo amesema hayo
jijini hapa leo katika ufunguzi wa mkutano wa Makatibu wakuu wa nchi za SADC
wanaoshughulikia na sekta za Mazingira,Maliasili na Utalii.
Amesema kuwa katika mkutano huo ambao ni sehemu ya
maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wanaosimamia sekta hizo katika nchi
wanachama, watajaribu kushawishi nchi wanachama waridhie itifaki hiyo ambayo
ina umuhimu mkubwa kutokana na nchi hizo kushirikiana katika kutunza rasilimali
zinazovuka mipaka kati ya nchi nan chi.
“Pamoja na kwamba kikao cha viongozi wakuu kilipitisha
itifaki hii mwaka 2014,ni nchi tatu tu zilizoridhia itifaki hii muhimu hasa
ikizingatiwa katika masuala ya mazingira tuna share resources (Tunashirikiana
katika masuala mengi ya rasilimali)  nyingi sana,mfano Ziwa Tanganyika lipo
Tanzania,Jamhuri ta Kidemokrasia ya Congo,Mto Zambezi ambao unapita katika nchi
kama tano za SADC.
 “Kwa hiyo kuna
umuhimu wa kukaa pamoja na kuangalia namna bora ya kutunza, kwa pamoja,
mazingira  yanayozunguka rasilimali hizo
kwa ajili ya maendeleo endelevu ya nchi wanachama na Jumuiya,” alisema Katibu
Mkuu huyo.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo Profesa
Adolf Mkenda ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii anasema mkutano
huo utajadili mambo mengi ikiwamo kupambana na ujangili, mkataba wa kimataifa
wa kulinda viumbehai na mimea iliyo katika hatari ya kutoweka(CITES) ambao
unakataza na kuruhusu uuzaji wa nyara zinazotokana na wanyamapori.
”Tunakutana kujadili  mambo mengi kuhusu mazingira,maliasili na
utalii hasa ushirikiano katika mapambano dhidi ya ujangili pamoja na kuandaa
ajenda kwa ajili ya mkutano wa mawaziri wa sekta hizo wa SADC ambao utafanyika
hapa, “anasema Profesa Mkenda
Aliongeza kuwa katika mkataba wa CITES kuna mjadala
mkubwa unaoendelea miongoni mwa wadau ambapo baadhi ya vipengele vinaonekana
kuchomekwa  kinyume cha utaratibu,hivyo
mkutano huo utajadili na kutoa mapendekezo ya vipengele hivyo
 “Kwa mfano kuna mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayotumika
kupiga kampeni ya kuzuia uvunaji halali wa mazao ya wanyamapori na kupinga
bidhaa kuingia sokoni jambo ambalo tunadhani si sahihi,na hilo ni moja ya
maeneo tutakayoyajadili na kuyatolea mapendekezo,” alisisitiza Profesa Mkenda
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kilimo,Chakula na
Maliasili katika Sekretarieti ya SADC, Domingos Gove,amesema Mkutano huo ni wa
kikatiba na wa kawaida unaofanywa na wataalamu mbalimbali katika nchi za
SADCkwa ajili ya kujadili changamoto na mafanikio yaliyorifikiwa nan chi wanachama

Mkutano wa Mawaziri wa sekta za Mazingira,Maliasili na
Utalii wan chi wanachama wa SADC utafunguliwa ijumaa wiki hii na Makamu wa Raiswa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Hassan Suluhu

Baadhi
ya Washiriki wa Mkutano huo wakifutilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof Adolf Mkenda (hayupo
pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho .
Mkurugenzi
wa Idara ya Chakula ,Kilimo na Maliasili wa  Sekretarieti ya SADC
,Domingos Gove akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
unaoshirikisha Makatibu Wakuu kutoka nchi 16 za SADC.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifutilia hotuba iliyokuwa
ikitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof Adolf
Mkenda (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho .
Baadhi ya Makatibu Wakuu wanaoshiriki Mkutano huo. 
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,prof ,Adolf Mkenda akizungumza na
Wanahabari mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa Makatibu
Wakuu wa Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za SADC.
Mkurugenzi
wa Idara ya Chakula ,Kilimo na Maliasili wa Sekretarieti ya
SADC,Domingos Gove akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufunguliwa
rasmi kwa mkutano wa
Makatibu Wakuu wa Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za
SADC. 

 
Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira ,Joseph
Malongo akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa
mkutano wa
Makatibu Wakuu wa Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za
SADC.
Makatibu
Wakuu na Maafisa Waandamizi  wa Sekta ya Mazingira,Maliasili na Utalii
wa nchi za SADC ,wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa
mkutano huo unaofanyika kituo cha kimataifa cha Mikutano cha AICC jijini
Arusha.