Ndege ya bek air iliyobeba watu 98 yaanguka na kuua 15

Takriban
watu 15 wamefariki baada ya ndege iliokuwa ikiwabeba abiria 98 na
wafanyakazi kuanguka nchini Kazakhstan , kulingana na maafisa wa uwanja
wa ndege wa nchi hiyo.


Wanasema kwamba ndege hiyo ya Bek Air ilianguka muda mfupi baada ya kupaa katika uwanja wa Almaty mapema siku ya Ijumaa.

Takriban watu 35 , ikiwemo watoto wanane walipelekwa hospitali. Ndege hiyo ni ya aina ya FlightZ92100.

Ndege hiyo ilikuwa ikielekea katika mji mkuu wa Kazakhstan wa Nursultan kutoka mji mkubwa wa Almaty.

Inadaiwa
kwamba kwamba ndege hiyo ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa moja na
dakika 22 , kabla ya kugonga kizuizi kimoja na kuangukia nyumba ya
ghorofa mbili.

Ndege hiyo haikuwaka moto baada ya kuanguka. Tume maaluma itabuniwa ili kubaini chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo.