Ofisi yavunjwa, nyaraka mbalimbali zikiwemo fomu za uchaguzi zaibiwa

Mnamo
tarehe 31.10.2019 majira ya saa 19:50 usiku huko Kijiji cha Pashungu,
Kata ya Itawa, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa
Mbeya. JACKSON MATONYA [28] Afisa mtendaji wa Kijiji cha Pashungu, mkazi
wa Pashungu aligundua kuvunjwa ofisi ya Kijiji cha Pashungu na kuibiwa
nyaraka mbalimbali kama ifuatavyo;

1. Fomu za wagombea wenyeviti wa vijiji na vitongoji.
2. Fomu za wajumbe wa kundi maalum la wanawake zilizojazwa 21 za
wagombea wa chadema 7 za wagombea wa ccm.
3. Fomu 24 za wenyeviti wa vijiji na vitongoji ambazo hazijajazwa.
4. Fomu 46 za kundi maalum la wanawake ambazo hazijajazwa.
5. Mhuri wa msimamizi msaidizi wa uchaguzi.
6. Faili moja la mihtasari ya malipo ya walengwa wa TASAF.
7. Faili la mihtasari ya vikao vya Halmashauri ya Kijiji na mikutano ya hadhara.
 
Kutokana na tukio hilo, jumla ya watuhumiwa nane [08] wamekamatwa ambao ni:-
1. MWAWA POSTA [40] katibu wa CHADEMA Kata ya Itawa
2. ENOCK JECK MWASILE [25]
3. ALEX JECK MWASILE [21]
4. AMONI SIFUKU MWASILE [40]
5. ALUWA JOHN NGELEKA [37]
6. BAHATI SIFUKU YANJILWA [45]
7. MOSKO ALLAN MWASELE [32]
8. CHARLES MANGENI MWASILE [31] wote wakazi wa Kijiji cha Pashungu.