Picha : nyoka mkubwa avamia mkutano wa waziri mkuu iringa…..askari polisi aliyemdhibiti apewa zawadi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemzawadia
Askari Polisi PC Alphonce Daniel Mwambenga sh. 200,000 kutokana na
ujasiri wake wa kumdhibiti kwa kumkanyaga nyoka mkubwa aliyekuwa
akieleakea jukwaa kuu wakati Waziri Mkuu akihutubia katika Kilele cha
Wiki ya Viziwi Duniani kwenye Uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini
Iringa, Septemba 28, 2019. 

Kitendo hicho kilifanyika kimyakimya
hivyo hapakuwa na taharuki yoyote . Pichani, Mheshimiwa Majaliwa
akimkabidhi Mwambenga fedha hizo. Wapili kulia ni Mke wa Waziri Mkuu,
Mama Mary Majaliwa, kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella
Ikupa na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara y a Elimu, Sayansi na
Tekinolojia, Dkt.Avemaria Semakafu. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Iringa, Ally Happy na wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Iringa, Dkt. Abel Nyamkahanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)