Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare wakati akikagua Mtambo Mtambo wa Kuchuja Chumvi “Reverse Osmosis” uliogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 2.3 utakaotumika kwa Mradi wa Maji wa Gairo, mkoani Morogoro. |
Waziri wa Maji, Prof. Makame
Mbarawa akitoa maelekezo ya kumaliza kazi ya Mradi wa Maji wa Gairo kwa
Wakandarasi wa Kampuni ya Protecno Srl ya Italia wanaosimamia kazi ya
ufungaji wa mtambo a pampu za kusukuma maji.

Mbarawa akiwa na baadhi ya wageni wa meza kuu katika hafla ya kupokea
Mtambo wa Kuchuja Maji ya Chumvi “Reverse Osmosis” kwa ajili Mradi wa Maji wa Gairo, mkoani Morogoro.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA), Mhandisi Tamim
Katakweba akitambulisha timu ya wataalam itayokuwa ikisimamia uendeshaji
wa Mtambo wa Kuchuja Maji ya Chumvi “Reverse Osmosis” kwa ajili Mradi wa Maji wa Gairo, mkoani Morogoro.

Sehemu ya Mtambo wa Kuchuja Maji
ya Chumvi (Reverse Osmosis) uliogharimu Sh. bilioni 2.3 utakaotumika
kwenye Mradi wa Maji wa Gairo, wilayani Gairo, mkoani Morogoro.

Sehemu ya Mtambo wa Kuchuja Chumvi “Reverse Osmosis” uliogharimu Sh. bilioni 2.3 utakaotumika kwenye Mradi wa Maji wa Gairo, wilayani Gairo, mkoani Morogoro.
Waziri wa Maji, Prof. Makame
Mbarawa amesisitiza Serikali itachukua hatua zozote zinazostahili ili
kumaliza kabisa tatizo la maji kwa wananchi katika maeneo yote yenye
changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji ikiwemo Wilaya ya Gairo,
mkoani Morogoro.

Kauli hiyo imekuja akiwa katika Wilaya ya Gairo kukagua Mtambo wa Kuchuja Chumvi (Reverse Osmosis)
uliogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 2.3 uliowasili kutoka nchini
Italia utakotumika kwenye Mradi wa Maji wa Gairo akitimiza ahadi
aliyoitoa alipokuwa ziarani mkoani Morogoro miezi michache iliyopita.

Prof. Mbarawa amesema Serikali
imetumia gharama kubwa kununua mtambo huo kwa kuwa inawathamini
wananchi wake na haitasita kuchukua hatua zozote zinazostahili katika
kutimiza azma yake ya kufikisha asilimia 85 ya upatikanaji wa maji
vijijini na asilimia 95 mijini ifikapo mwaka 2020.

Pia, amesisitiza pamoja na
kufungwa kwa mtambo huo, inafanya utaratibu wa kutafuta chanzo kingine
cha maji kitakachoongeza uzalishaji wa maji yatakayotosheleza na
kumaliza tatizo la Maji kwa Mji wa Gairo.

Prof. Mbarawa amesema ifikapo
mwezi Novemba, 2019 mradi utaanza kutoa huduma kwa wananchi na kumtaka
Mkandarasi, Kampuni ya Protecno Srl ya Italia kumaliza kazi ya ufungaji
wa mtambo na pampu haraka.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro, Loata Ole Sanare ameishukuru Wizara ya Maji kwa kuchukua hatua
ya kuukamilisha mradi huo ambao umechukua muda mrefu na kutimiza ahadi
ya kuleta mashine hiyo itakayoimarisha kiwango cha ubora wa maji, ambayo
kwa maeneo ya Gairo yana changamoto kubwa ya chumvi nyingi.

Akisisitiza Serikali imepeleka
takribani Shilingi bilioni 16 katika Wilaya ya Gairo kwa dhamira ya
kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji na kuishukuru Serikali kwa niaba
ya wananchi wa Gairo kwa kusikia kilio chao cha mahitaji ya huduma ya
majisafi na salama, hususan kwa Mji wa Gairo unaokua kwa kasi wenye
wakazi wapatao 55,000.

Miongoni mwa wakazi wa Gairo
wamesema kuwasili kwa mashine hiyo, ambapo baadhi yao walidiriki
kudhihaki kuwa ahadi ya Waziri wa Maji ni porojo kwa kuwa wameshaahidiwa
ahadi lukuki bila kutimiziwa, wamesema hakika Serikali imedhamiria
kutatua kero ya maji katika wilaya yao yenye tatizo kubwa la maji
kulinganisha na maeneo mengine Morogoro huku wakisema wanasubiri kwa
hamu kubwa maji hayo ifikapo mwezi Novemba ili waweze kufurahia matunda
ya Serikali yao.

Ujenzi wa Mradi wa Maji wa
Gairo unatekelezwa kwa pamoja na wakandarasi wa Kampuni za Serengeti Ltd
na Protecno Srl chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingira Morogoro (MORUWASA) kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni
10, umelenga kuhudumia wananchi wapatao 32,808 na utainua kiwango cha
upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 38 kwa sasa mpaka asilimia
80 utakapokamilika.