Rc mndeme afanya ziara wilaya ya kishapu, atoa maagizo kwenye miradi ya maendeleo


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon
Mndeme ameendelea na ziara zake ambapo  Jumatatu Oktoba 30,2023 ametembelea
na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Mkoani Shinyanga.

Mhe. Mndeme pamoja na kupokea taarifa za miradi ya
maendeleo amesikiliza na kupokea kero za wakazi wa Wilaya ya Kishapu huku
akiwaelezea hatua mbalimbali za maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga  ambapo amewaomba kuendelea kuiunga mkono
serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika
shughuli za maendeleo.

RC Mndeme amekagua ujenzi wa jengo jipya la ofisi ya
mkuu wa Wilaya ya Kishapu linalotekelezwa kupitia fedha za serikali zaidi ya
Bilioni moja ambapo ametoa wiki mbili mradi huo uwe umekamilika.

Awali katika taarifa ya mradi iliyosomwa na katibu
tawala wa Wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed mradi huo upo katika hatua ya
ukamilishaji na kwamba ulianza Mwezi Machi 3,2022.

Mhe. Mndeme ametembelea nyumba mpya ya mkuu wa
Wilaya ya Kishapu inayojengwa kupitia fedha za serikali kuu ambapo pia ametoa
wiki mbili mradi huo we umekamilika ili shughuli za taratibu zingine za
maendeleo ziweze kuendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme katika
ziara yake ya leo amekagua ujenzi jengo la huduma jumuishi (One stop Center)
katika Hospitali ya Wilaya mradi huo unatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu
kwa kushirikiana na shirika la UNFPA.

Mndeme amekagua na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi
wa mradi wa maji ya ziwa Viktoria Seseko – Ngundangali unaotekelezwa kwa fedha
za Serikali Kuu kupitia mradi wa P4R mradi huo unatekelezwa kwa muda wa mwaka  mmoja ambapo   ulianza 
kujengwa  Tarehe 30 Machi ,
2023  na 
unatarajiwa   kukamilika  Mwezi Machi, 
2024.

Akisoma taarifa fupi ya mradi huo wa maji ya Ziwa
Viktoria Seseko – Ngundangali, meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu mhandisi
Dickson Kamazima ameeleza lengo la mradi huo ambapo amesema wananchi 15,500
watanufaika na mradi huo.

“Muda
wa  utekelezaji   Mradi 
siku 365  sawa  na 
mwaka  mmoja ,  Mradi 
ulianza  kujengwa  Tarehe 30 Machi , 2023  na 
unatarajiwa   kukamilika  Mwezi Machi, 
2024.”

“Lengo
la mradi hu ni kumtua mama ndoo kichwani, kwa kumpunguzia umbali wa kufuata
maji na kumuongezea muda wa kushiriki shughuli za kiuchumi na kijamii, pia
kupunguza magonjwa yanayosababishwa na kutumia maji yasiyo safi na salama”.
Amesema
mhandisi Kamazima  

“Kazi
zilizopangwa kutekelezwa katika Mradi huu, ni ujenzi wa matangi matatu (3) ya
kuhifadhi maji yenye ujazo wa lita 200,000 kwenye minara wa mita 15 pamoja  na uzio, kutandaza mtandao wa bomba umbali wa
Kilomita 41.5na kujenga vituo vya kuchotea maji (DPs) 31. Kazi zote
zimekamilika kwa asilimia 95 (95%)”.

“Gharama
ya Mradi ni Tsh 2,810,058,195.00 ikijumuisha Kodi ya ongezeko la Thamani (VAT) ambazo
ni fedha kutoka Serikali kuu, kuptia Program ya Malipo kwa Matokeo (Payment for
Result), hadi sasa Mkandarasi ameshalipwa  
kiasi cha Tsh 330,495,816.25”.
Amesema mhandisi
Kamazima

“Wanufaika
wa mradi huu ni wananchi wa vijiji vitano (5) vya Ngundangali, Dugushilu,
Kakola, Seseko na Mpumbula wapatao 15,500”

“Kwa
niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Kishapu, nachukua fursa hii kuishukuru Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Mhe: DKT Samia Suluhu
Hassan kwa jitihada zake za kutupatia fedha za ujenzi wa Miradi ya maji katika
Wilaya ya Kishapu”.
Amesema mhandisi Kamazima

Mhe. Mdeme amekagua ujenzi wa nyumba mbili (2) za
walimu (2 in 1) katika shule ya sekondari Bupigi zinazojengwa kupitia mradi wa
SEQUIP na kwamba mradi huo upo hatua za ukamilishaji.

Lakini pia mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina
Mndeme amekagua ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Jitegemee (Nguzombili)
iliyopo  kata ya Maganzo ambapo ujenzi
huo unatekelezwa kupitia mradi wa BOOST.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.
Joseph Mondest Mkude amesema Wilaya hiyo kupitia serikali itaendelea kutatua
changamoto zilizopo ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.

Ameeleza kuwa katika miradi inayotekelezwa Wilaya ya
Kishapu inaendelea kusimamia upatikanaji wa mafundi waaminifu katika
utekelezaji wa miradi hiyo ambapo amesema wanaendelea kushirikiana na wadau wote
wa maendeleo katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi.

DC Mkunde ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa
fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Kishapu
nachukua fursa hii kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa juhudi anazoendelea nazo za kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga
miradi ya Maendeleo (Maji Mijini na Vijijini, Ujenzi wa vituo vya Afya,
Barabara, Vyumba vya madarasa kwa shule za Msingi na Sekondari na miradi
mikubwa ya kimkakati”.

“Watumishi wote Tunamuahidi kuwa tupo pamoja nae
katika kusimamia miradi ya maendeleo na kuakisi utendaji wake wa kazi
uliotukuka”.
amesema DC
Mkude

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Mhe. Christina Mndeme leo Jumatatu Oktoba 30,2023 amefanya ziara ya siku moja
kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Kishapu
akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo kamanda wa jeshi la Polisi
Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon
Mndeme akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali katika zoezi la kutembelea ujenzi
wa nyumba  mpya  ya mkuu wa Wilaya ya Kishapu Jumatatu Oktoba 30,2023.


Wananchi wa Ngundangali, Dugushilu, Kakola, Seseko
na Mpumbula 

Wananchi wa Ngundangali, Dugushilu, Kakola, Seseko
na Mpumbula