Rc sanare apiga rungu waalimu kuhamia mjini


Na farida saidy, Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Loata
Ole Sanare amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhandisi  Emmanuel
Kalobelo kuhakikisha anasimamia vyema na kusitisha mara moja swala la
watumishi wa Umma kuhamishwa kiholela kutoka maeneo yao ya kazi vijijini
na kuhamiashiwa mjini hususani katika sekta ya elimu.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amesema
hayo wakati akizungumza  na watumishi wa halmashauri ya Manispaa Ya
Morogoro ambapo amemtaka Katibu Tawala huyo kuhakikisha watumishi
waliozidi katika maeneo mbalimbali wahamishwe ili kupelekwa vijijini ili
kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi.
pia Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa
watumishi wa idara ya elimu wahakikishe wanafunzi wote waliofaulu
mtihani wa darasa la saba wanapata nafasi ya kujiunga na kidato cha
kwanza huku akiwataka watumishi wa sekta hiyo kuwa tayari kuwapokea
wanafunzi hao.
kwa upande wake katibu tawala Mkoa
wa Morogoro Mhandisi Emmanuel kalobelo akawata watumishi hao kufanya
kazi kwa uadilifu na umoja ili kutatua changamoto zilizopo huku mstahiki
meya wa Manispaa ya Morogoro akiwataka watumishi na wananchi kuwa
wawazi kwa kila mmoja wao.