Serikali yaagiza maduka ya pembejeo za kilimo yakaguliwe shinyanga


Mkuu wa mkoa wa Shinyang Mhe. Zainab Telack

Na Salvatory Ntandu – Malunde 1 blog
Serikali Mkoani Shinyanga imeagiza kufanyika kwa ukaguzi wa maduka yote
pembejeo za kilimo mkoani humo baada ya kubainika kuwepo kwa yanayouza
dawa na pembejeo ambazo hazina ubora kabla ya msimu wa kilimo ambao
unataraji kuanza hivi karibuni.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri na
maendeleo ya mkoa wa Shinyanga (RCC),ambaye pia ni mkuu wa mkoa huo
Zainab Telack  ambapo amesema Maafisa (TFDA) na (TBS) wanapaswa kufanya
kazi hiyo kwa haraka ili kuwawezesha wakulima kupata pembejeo bora.
Amesema baadhi ya wamiliki wa maduka ya pembejeo mkoani humo wamebainika
kuuza pembejeo zisizokizi viwango kama vile mbegu na dawa ambazo
zimeshakwisha muda wake na kusababisha wakulima kupata hasara kwa
kutoota pindi wanapopanda.
Telack amefafanua kuwa endapo hatua za haraka zisipochukuliwa kwa
wamiliki hao wataendelea kujinufaisha wao wenyewe na kuisababisha
malalamiko kutoka kwa wakulima hivyo mamla husika zinatakiwa kuwa
makini.
Sanjari na hilo Telack amesema kuna baadhi ya maduka yapo katika mkoa wa
shinyanga na hayana usajili kutoka mamlaka husika na wanaendelea kutoa
huduma jambo ambalo ni kinyume na sheria na wanaweza kuhatarisha
usalama wa wakulima pindi wanapowapa huduma.
Naye Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad
ameshauri ukaguzi huo uwe ni endelevu na TFDA na TBS ni lazima
wahakikishe watumishi wanaouza maduka hayo wawe na sifa zinazotakiwa kwa
mujibu wa leseni zao.
Ameongeza kuwa wapo baadhi ya wamiliki wa maduka hayo wamekuwa wakiwapa
watu wasio kuwa na sifa kuuza maduka ya pembejeo hali ambayo inaweza
kusababisha wakulima wakapata hasara kutokana na kutokuwepo kwa umaki
katika utoaji huduma.
Amefafanua kuwa katika mkoa wa shinyanga baadhi ya mifugo imebainika
kupewa chanjo ambazo hazina ubora na kusababisha mifugo kufa na mbegu
kutoota jambo ambalo lisipochukuliwa hatua za haraka linaweza kuleta
madhara kwenye jamii.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza
Wadau wakiwa ukumbini.