Shuwasa yawatoa hofu wateja wake huduma ya maji kurejea muda wowote mjini shinyanga

Afisa mahusiano na mawasiliano SHUWASA Bi.
Nsianeli Gelard (Manka) akizungumzia changamoto ya kukatika kwa huduma ya maji.

Na Mapuli
Misalaba, Shinyanga

Wakazi wa Manispaa
ya Shinyanga wamesema hali ya kukatika kwa maji mara kwa mara imekuwa
ikisababisha usumbufu kwa watumiaji wa huduma hiyo majumbani na kwenye maeneo
ya Biashara.

Wamelalamikia hali
hiyo wakidai kuwa ni usumbufu na kwamba imekuwa ikisababisha hatari katika
uendeshaji wa shughuli za kibiashara ambazo zinategemea huduma ya maji.

Wameiomba mamlaka
ya maji safi na usafi wa mazingira Shinyanga SHUWASA kutoa ratiba ya uhakika
ili kuwawezesha watumiaji kuhifadhi maji ya kutosha,kuliko hivi sasa ambapo
taarifa zinazotolewa zinakuwa hazieleweki.

Kutokana na
malalamiko hayo Afisa mahusiano na mawasiliano SHUWASA Bi. Nsianeli Gelard
ambaye ametoa ufafanuzi juu ya changamoto hiyo.

“Tulikuwa na changamoto ya huduma ya maji kwa Manispaa
ya Shinyanga pamoja na miji midogo ya Tinde, Didia na Iselamagazi  changamoto hiyo ilianza tarehe nne mpaka
tarehe nane lakini ilitokana na wenzetu wa mamlaka ya maji safi na usafi wa
mazingira KASHUWASA  walikuwa wameacha
uzalishaji wa mitando yao ya maji katika mitambo yao ya maji  iliyopo Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza
kutokana na majaribio ya mfumo mpya ya kuweka dawa zoezi hilo lilichukua
takribani siku tatu baada ya hapo huduma ilirejea kama kawaida”.amesema Nsianeli

“Tarehe tisa tulipata tena changamoto katika mradi huo
wa uzalishaji maji wa KASHUWASA ambapo nguzo za umeme zilianguka na wataalam wa
TANESCO walikuwa wanaendelea na marekebisho lakini hadi kufikia leo asubuhi
huduma ilikuwa bado haijarejea, lakini muda huu tumefanya mawasiliano na watu
wa tenki la Old Shinyanga wamesema maji yameanza kuongia ingawa yanamgandamizo
kidogo”.

“Tukirudi kwa upande wetu SHUWASA tuna bwawa la Nhimwa
kwa tarehe 4 mpaka 8 tulikuwa na changamoto ya mifumo ya mashine zilizopo pale
lakini juhudi zilifanyika mpaka tarehe 8 asubuhu tuliweza kuzalisha maji yetu
ya Nhimwa lakini isipokuwa jana usiku umeme katika maeneo ya mitambo ya Nhimwa
hakuna kwahiyo uzalishaji umesimama mpaka sasa”.amesema Nsianeli

Afisa mahusiano na
mawasiliano SHUWASA Bi. Nsianeli Gelard (Manka) amewatoa hofu wateja wake huku
akieleza kuwa juhudi mbalimbali za kurejesha huduma zinaendelea.

Akizungumzia
changamoto hiyo  mhandisi wa mipango
kutoka shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa Shinyanga Hassan Koko amesema
changamoto hiyo inatafutiwa ufumbuzi wa haraka ili wananchi waweze kupata
huduma ya maji.

“Kweli tunachangamoto ya umeme
maeneo ya kuanzia Nhimwa kuelekea Mwakitolyo mpaka Iselemagazi Old Shinyanga na
hii changamoto imetokana na nguzo yetu moja kubwa ya laini kubwa ilipata
hitilafu jana usiku saa tisa kwa kukatika upande wa juu mpaka sasa mafundi wapo
saiti wanaendelea na kazi matumaini yetu ifikapo jioni kazi itakuwa imekamilika
na wateja wetu watapata huduma ya umeme”.amesema Mhandisi Koko

 Afisa mahusiano na mawasiliano SHUWASA Bi.
Nsianeli Gelard (Manka) akizungumzia changamoto ya kukatika kwa huduma ya maji.

Mhandisi wa
mipango kutoka shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa Shinyanga Hassan Koko
akititolea ufafanuzi changamoto hiyo.