Taarifa ya ongezeko la hali ya joto kwa baadhi ya maeneo nchini.

Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kutakua na ongezeko la joto
katika baadhi ya maeneo nchini, kufuatia kuwepo kwa hali ya unyevunyevu
angani.

TMA imeyataja maeneo yatakayoathirika zaidi ni ukanda wa pwani
yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha joto cha nyuzi joto 32 hadi
34 hususan kwa maeneo ya Dar es Salaam, Tanga, Unguja na Pemba.

Taarifa kwa umma iliyotolewa jana Jumanne, Januari 7, 2020 na Mkurugenzi
Mkuu TMA, Dk Agnes Kijazi imeeleza kwa kawaida kipindi cha Oktoba hadi
Machi kila mwaka 2020 jua la utosi linakuwa katika maeneo ya kizio cha
kusini mwa dunia.

Amesema Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizopo katika kizio cha kusini,
huwa na hali ya joto kali katika maeneo mengi ikilinganishwa na miezi
mingine.