Afisa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Rolf Kibaja ,akizunguza na wanahabari kuacha mihemko badala yake waandike habari zenye ulinganifu.

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kufanyakazi zao kwa kufuata kanuni mpya zilizoongezwa kwenye sheria mpya ya EPOCA, na kuacha kufanya shughuli zao kwa ushabiki ili kusaidia wanachi kupata taarifa zilizofanyiwa kazi na ambazo zipo katika mrengo sahihi.
Akizungumza kwenye semina ya siku moja iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na TCRA kwa wanahabari Mkoani humo, Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu alisema ni vyema kwa Sasa waandishi wa habari katika shughuli zote wanazozifanya za uandishi ziwe zinaendana na sheria kanuni na taratibu zote walizowekewa ili kuepuka kuingia kwenye migogoro ya kisheria na Mamlaka za Serikali.
Gwandua Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA)na kusema kuwa mwandishi anahitajika kupewa elimu ,na kukumbushwa masuala yanayogusa moja kwa moja ,katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku.
Mtoa mada katika semina hiyo Afisa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Rolf Kibaja ,aliwataka wanahabari kuacha mihemko badala yake waandike habari zenye ulinganifu,mizania na kwa ufasaha sambamba na kujiepusha na maoni yao binafsi.
Kibaja aliwakumbusha waandishi kuwa Tume ya uchaguzi ndiyo yenye jukumu la kutoa matokeo ya uchaguzi ,na siyo wao kujitwika majukumu ambayo siyo ya kwako,alisisitiza endapo kutakuwa na tashwishwi yeyote ni vyema wakapata majibu sahihi kutoka kwa tume yenyewe
Aliwasihi wanahabari kuzingatia na kufuata kanuni na maadili maudhui mtandaoni ,pamoja na kuhakikisha habari kabla haijapelekwa kwa walaji lazima iwe na usawa pande zote mbili, ili kuleta tija katika jamii bila kusahau kuzingatia kanuni ya uchaguzi ya mwaka 2020 namba 343.
Kwau wake Makamu mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoani Arusha Musa Juma, aliwasilisha mada isemayo usalama wa waandishi kazini na mitandao ya kijamii ,ambapo alisema kuwa mitandao ya kijamii ina faida na hasara zake, hivyo aliwataka wanahabari kuacha kuweka taarifa zao muhimu katika mitandao hiyo ,kwani ni rahisi mtu yeyote kuwafuatilia na hata kudhurika pia
Aliwataka kufahamu kuwa kwa miaka ya sasa ni vigumu sana kuishi bila kutumia intaneti ,kwa namna moja ama nyingine bali intaneti hiyo ina madhara pia ,kwa mfano: kukumbana na taarifa za uongo,kichaka cha uhalifu, hurahisisha udanganyifu wa taaluma,pia ni chanzo cha kusambaa kwa virusi vya kompyuta.
Musa alisema kuwa mitandao hiyo ikitumika vizuri zipo fursa mbalimbali za kufungua milango mipya ya chombo kingine cha habari,pia imeweza kuwaleta watu wengi kwa karibu zaidi ila tahadhari ni muhimu mno ,haswa kwa waandishi kwani maisha yao yana thamani kubwa kuliko kitu chochote kile ,hivyo ni vyema wakaitumia kwa umakini wa hali ya juu.
Hivyo aliwataka waandishi wa habari kutawala matumizi yao pamoja na kuzingatia kanuni za usalama kwenye mitandao ili wasiathirike .