Tumieni fursa hizi mlizozipata katika kukuza sekta ya uvuvi -gekul

 

  Naibu
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Pauline Gekul akizungumza
katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi nchini uliofanyika kwa siku
tatu katika ukumbi wa mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
JNICC Jijini Dar es Salaam. Waziri
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akizungumza katika
Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi nchini uliofanyika kwa siku tatu
katika ukumbi wa mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNICC
Jijini Dar es Salaam.


Waziri mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo
Pinda akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi nchini
uliofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mkutano wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam. Katibu
Mkuu wa Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah akizungumza katika Mkutano
wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi nchini uliofanyika kwa siku tatu katika
ukumbi wa mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNICC Jijini
Dar es Salaam. Mkuu
wa Mkoa Mstaafu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Sadick Meck Sadick
akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi nchini uliofanyika
kwa siku tatu katika ukumbi wa mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam.


(Picha na Emmanuel Mbatilo)




NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


Wadau wa sekta ya Uvuvi nchini
wametakiwa kutumia fursa zinapojitokeza katika sekta hiyo ili kuweza
kukuza uchumi wakati huo huo wakihakikisha wanatokomeza uvuvi haramu.


Ameyasema hayo jana Naibu Waziri
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Pauline Gekul alipokuwa anafunga
Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi nchini uliofanyika kwa siku tatu
katika ukumbi wa mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNICC
Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza wakati anafunga
mkutano huo Mhe.Gekul alisema kupitia mkutano wa wadau wa uvuvi wameweza
kuibua fursa mbalimbali zinazohusiana na Uvuvi hivyo wadau wakitumia
vizuri fursa hizo wanaweza kunufaika.


“Moja ya fursa ambayo wameza
kuibua ni pamoja na uwekezaji katika bahari kuu, tumeona TAFICO
inavyokwenda kufufuliwa pamoja na ujenzi wa bandari ya Uvuvi Mbigani
Bagamoyo pamoja na kununua meli 4 na kwa ujumla zinakuwa 8 na Zanzibar
kwaajili ya kuanza uwekezaji katika bahari kuu”. Alisema Mhe.Gekul.


Aidha Mhe.Gekul alisema wameweza
kufahamu mahitaji ya vyakula vya samaki kwamba nikiasi gani wajiandae
kuelekea kwenye kilimo cha ufugaji wa samaki katika mizimba pamoja na
mabwawa.


“Tunapoelekea kukuza sekta ya
uvuvi ni vizuri tukatumia fursa ya upatikanaji wa dhana bora ya uvuvi
ili kuweza kuwanufaisha wavuvi pamoja na wananchi kwa ujumla na kuweza
kukuza uchumi”. Alisema.


kwa upande wake Katibu Mkuu wa
Wizaya Viwanda na Biashara amesema kuwa katika wiki mbili zilizopita
kulitokea taarifa ya samaki kuonekana wamekufa katika maeneo mbalimbali
ya ziwa Victoria na kuwapa watu hofu ya uwezekano wa samaki wale kuwa na
sumu, hivyo kukatumwa timu ya maabara kwaajili ya kujiridhisha na
majibu yalivyotoka ikaonekana kuwa hawakuwa na sumu.


“Baada ya hofu kutokea nilituma
timu yangu ya maabara na kuchukua sampo ya samaki katika maeneo ya
Rorya, Musoma, Mwanza,Sengerema na Bukoba tukazipeleka kwa mkemia mkuu
ili aweze kuangalia kama kuna sumu au wamekufa kwa mabadiliko ya tabia
nchi”.


Amesema matokeo yalivyotoka na kuonesha kwamba sampo zote za samaki walizopeleka hakuna samaki yoyote aliyekutwa na sumu.


” Kuna hali huwa inajitokeza
ziwani kwenye miezi ya baridi ambayo inafanya maji ya juu kupata baridi
na kuwa nyuzi joto sawa na yale ya chini hivyo ikitokea upepo maji ya
chini yanakuja juu na kuchanganyikana na kusababisha baadhi ya samaki
kufa”. Amesema