Ubalozi
wa Palestina nchini Tanzania unaangazia uhalifu wa Israeli dhidi ya
watu wa Palestina katika Yerusalem ya Mashariki iliyoko chini ya ukoloni
na ukalizi wa Israeli.
Yerusalemu
ya Mashariki ni sehemu muhimu ya nchi ya Palestina. Tangu kukaliwa
kwake na ardhi kuporwa kutoka kwa Wapalestina kinyume na sheria za
kimataifa mnamo mwaka 1967, Israeli imeweka lengo na utaratibu wa
kubadilisha hali ya kisheria ya jiji, kudhibiti na kubadilisha muundo wa
idadi ya watu waishio hapo.
Kupitia
sera za kibaguzi na kwa kukiuka sheria Za Kimataifa kama ilivyoelezewa
na ripoti ya Haki za Binadamu, iliyotoka hivi karibuni; Israeli ina nia
ya kuunda kwa makusudi, ukweli mpya juu ya ardhi ya Wapalestina.
Kuwezesha
hilo, Israel imekuwa ikihamisha maelfu ya mamia ya watu wa Palestina
kwa nguvu na kuwaondosha katika makazi yao ya miaka mirefu na kisha
kuikabidhi kwa walowezi wa Israeli. Zaidi ya walowezi 200,000 wanaishi
katika makazi haramu mjini humo, Mashariki ya Yerusalem.
Israel
yaendelea na upanuzi wa makazi haya katika ardhi ya Wapalestina kama
ilivo sasa katika mtaa wa Sheikh Jerrah huko mjini Yerusalemu ya
Mashariki ampapo famia saba za Wapalestina zalazimishwa kuondoka katika
makazi yao.
HalikadhalikaIsraeli
katika harakati zake kuufanya mji wa Yerusalemu kuwa mji wa Kiyahudi
hufanya mashambulio yake ya kimfumo dhidi ya waumini wa Palestina wa
dini za Kikristo na Kiislamu. Jeshi la Israeli limekuwa likivamia na
kushambulia waamini wa Kikristo na Kiislamu hasa katika sherehe zao za
dini mjini Yerusalemu mashariki.
Wanajeshi
wa Israeli mara kwa mara huzuia waumini wa Kiislamu wa Palestina
kuingia ndani ya msikiti wa Al – Aqsa kwa ajili ya sala
Kulingana
na ripoti ya Human Rights Watch ambayo ilichapishwa mnamo mwezi Aprili
mwaka huu, Israeli inaendelea kuonyesha ukandamizaji na vitendo visivyo
vya kibinadamu dhidi ya watu wa Palestina kwa nia ya kudumisha utawala
wa kikabila unaowapa ukuu Wayahudi juu ya Wapalestina.
Ripoti
hiyo ilihitimisha kwa kusema kuwa, Israeli inatekeleza utawala katili
wa ubaguzi wa rangi ambao umesababisha miaka 54 ya ukoloni na makazi
haramu katika ardhi ya Palestina na hivyobasi kukiuka sheria na maazimio
ya Umoja wa Mataifa.
Ubalozi
wa Palestina nchini Tanzania unaangazia msimamo wa serikali ya
Palestina kuhusu unyama huu unaofanywa na Israeli dhidi ya Wapalestina.
Akiongea
na waandishi wa habari hivi leo, Balozi wa Palestina nchini Mh. Hamdi
Mansour AbuAli ameitaka jumuiya ya kimataifa kutokaa kimya mbele ya
uhasama na ukatili huu unaotendeka dhidi ya Wapalestina katika ardhi
yao.
Balozi
amesema kuwa huu ni wakati muafaka kwa hatua ya kimataifa kutumia njia
na hatua zinazoelezwa na sheria za kimataifa na hatimaye kuifanya
Israeli na mashirika ya walowezi kuwajibika kwa ukiukaji wao na uhalifu
dhidi ya watu wa Palestina.