Uwajibikaji chachu kuimarika jumuiya ya afrika mashariki na kuondoa changamoto ndogo ndogo za ukosefu wa fedha

Na Ahmed Mahmoud Arusha
 Image result for jumuiya afrika mashariki

Imeelezwa kuwa changamoto za
ukosefu wa fedha ndani ya Sekretariet ya jumuiya ya Afrika Mashariki
bado zipo ila sio kama ilivyokuwa awali.
Hayo
yalielezwa na Mbunge wa Bunge la EALA Mariam Ussi Yahaya baada ya
kutokea mjadala mkubwa wa suala la ukosefu wa fedha za kuendesha Jumuiya
hiyo ndani ya bunge la EALA baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya ukaguzi
wa fedha wiki iliyopita.
Alieleza
kwa hapo awali kulikuwa na ubadhirifu mkubwa Ila baada ya bunge
kuisimamia kidete ubadhirifu umepungua kwa kiasi kikubwa hivyo kuifanya
suala hilo kuweza kubana matumizi yanayosaidia kuendelea kwa shughuli za
kila siku kwa kuwa jumuiya bado ni ndogo hivyo changamoto ndogo ndogo
lazima ziwepo.
Alisema
kuwa ripoti hiyo ni nzuri tofauti na huko nyuma Ila inatakiwa kwenda na
muda halisi ipo nyuma miaka miwili tunahitajika kwenda na muda uliopo
kwa kuwa watu wapo kiuwajibikaji itasaidia kuondoa changamoto ambazo
zimebakia sio kama jumuiya imeshindwa kuondoa ubadhirifu ni muda tu
tutamaliza changamoto hii.
Kwa
mujibu wa mbunge huyo kuimarika kwa jumuiya na shughuli zake kunatokana
na Bunge hilo kuongeza usimamizi wake hivyo sio kwamba ubadhirifu
utaendelea kukua bali ndio wameendelea kusaidia kuondoa tatizo hilo
kuifanya jumuiya hiyo kuongeza ufanisi na kuimarika.
“Sioni
sababu ya kuendelea au kuweka sheria kali za kusimamia kwa kuwa jumuiya
hii inaendesha shughuli zake kwa maridhiano ya mkataba wake hivyo naona
jumuiya ikiendelea kuimarika siku hadi siku na ubadhirifu au ukosefu wa
fedha sio kikwazo wala changamoto kubwa kwa Sasa”
Kwa
Upande wake Mbunge wa Bunge hilo George Odongo alisema kuwa mjadala wa
ripoti ya ukaguzi wa Fedha utasaidia Sana kuongeza nidhamu na
uwajibikaji miongoni mwetu kusaidia kuongeza ufanisi na jumuiya
kuendelea kuimarika.
Alisema
kuwa msingi mkubwa wa jumuiya kuendelea ni kusimama na suala zima la
uwajibikaji na kutanguliza mapenzi makubwa ya mtangamano ambayo wananchi
wetu ndio waliotufanya tuwe hapa kuendeleza udugu utakaosaidia
kuendeleza Umoja wetu.
“Nakumbuka
Sana waziri wetu wa Uganda alisema hapa nchini Tanzania mwalimu Nyerere
aliwahi kusema watanzania wafunge mikanda ili kuweza kukomboa nchi zetu
za bara la Afrika Umoja ndio msingi wa waafrika kuweza kufanikiwa
kwenye jambo lolote nasi bunge tupo kuisimamia kuweza kuimarisha umoja
huu”
Akiongelea suala la
Muswada wa sheria ya madini ambayo bunge hilo limefikia mahali pazuri
kwa kuangalia sheria za Tanzania kama njia ya utungwaji sheria za
mataifa hayo ya jumuiya ya Afrika Mashariki na kusema sheria inaweka
wazi nchi yenye sheria nzuri zitumike na wanajumuiya.
Nae
Mbunge wa Eala Mhandisi Suzan Masay alisema kuwa suala la ukosefu wa
fedha ni pana linahitaji Baraza la mawaziri kulipatia ufumbuzi wa kudumu
ili kuona wafanyakazi wakipata stahiki zao Tena kwa wakati na
wafanyakazi waweze kuwajibika kuendelea kuimarisha misingi ya
uwajibikaji.
Alieleza
kuwa msingi mzuri wa wafanyakazi kupata.stahiki zao ndio jukumu la
kuendesha Jumuiya kwa kuwa kila mmoja kwa nafasi yake awe mtafiti aweze
kutekeleza ndani ya muda uliopangwa kusaidia shughuli za jumuiya
kutokwama hivyo suala hili liangaliwe kwa umakini mkubwa Sana.
Suala
la wafanyakazi ni suala gumu kidogo tumekuwa tukisubiri mabadiliko ya
kisheria ambayo yakikamilika yatasaidia kuondoa changamoto hiyo na
kuendelea kuimarisha misingi ya uwajibikaji ndani ya jumuiya yetu
tusubiri wakikamilisha suala hilo itakaa sawa.
“Jumuiya
yetu inaendesha shughuli zake kwa kutegemea michango kutoka kwa nchi
wanachama na wafadhili Sasa fedha zikiwa kidogo kutokana na michango ya
nchi hizo na wafadhili wakichelewesha fedha ndio changamoto inaanzia
hapo suala hili linazungumzika na kila hatua tunayopiga kama jumuiya
inahitaji maridhiano ya pamoja”