Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akipitia rekodi za ukusanyaji na
uingizaji wa mifugo mnadani katika mnada wa Pugu alipofanya ziara ya
kutembelea mradi huo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mnada wa Upili Pugu Jijini Dar es Salaam Bw.Kerambo Samweli akitoa
taarifa kuhusu uendeshaji wa mnada huo kwa Waziri wa mifugo na Uvuvi
Mhe.Mashimba Ndaki (hayupo pichani) mara baada ya Waziri kutembelea leo
mnada huo.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akisikiliza kero zinazowakumba
wauzaji wa mifugo katika mnada wa mifugo Pugu Jijini Dar es Salaam mara
baada ya kutembelea mnada huo leo . Wafugaji
na wafanyabiashara wa mifugo wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe.Mashimba Ndaki mara baada ya kutembelea mnada wa Mifugo Pugu leo
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akizungumza jambo na Mkuu wa
Mnada wa Upili Pugu Jijini Dar es Salaam Bw.Kerambo Samweli mara baada
ya Waziri kutembelea leo mnada huo. Waziri
wa mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akizungumza na baadhi ya viongozi
wa Mnada wa upili Pugu baada ya kutembelea mnada huo leo Jijini Dar es
Salaam.
(Picha na Emmanuel Mbatilo)
NA EMMANUEL MBATILO
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki ameelekeza Uongozi wa Mnada wa
Mifugo Pugu Jijini Dar es Salaam kufikia Juni mwaka huu kuweza kukusanya
mapato kufikia Bilioni 3 au zaidi.
Ameyasema hayo leo mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea mnada huo kuona maendeleo na changamoto zinazoukabili mnada huo.
Akizungumza
katika ziara hiyo Mhe Ndaki amesema ukusanyaji mdogo wa mapato
unaotokea katika mnada huo ni kutokana na uzembe unaofanywa na baadhi ya
viongozi wanaosimamia mnada huo.
“Nataka
tarehe 30 Juni makusanyo yenu yawe Bilioni 3 au zaidi ndicho
ninachotaka zaidi kwenye mnada huu, hayo ndio maelekezo yangu kwenu
tufanyeni kazi kwa uadilifu tuacheni hizi kona kona”. Amesema Mhe.Ndaki.
Pamoja
na hayo Mhe.Ndaki amewaahidi watumiaji wa mnada huo kuukarabati ili
kuweza kuondokana na kero zinazopatikana kwenye mnada huo hasa mifugo
kupotea kutokana na kutokuwepo kwa uzio (ukuta) pamoja na ukosefu wa
maji kwaajili ya mifugo.
“Mnada
huu tutaukarabati miundombinu ya mnada huu kwasababu unatuingizia fedha
nyingi, hatuwezi kukosa fedha ya kuweka tofali na ukuta kuzunguka mnada
huu angalau tutaanza na hilo na mengine yatafuata ikiwemo maji kwaajili
ya mifugo”. Amesema
Aidha
amewataka wafanyabiashara na wafugaji kuendelea kufanya kazi kwa uhuru
kwani viongozi wa Serikali watendelea kuondoa changamoto ambazo
wanakutana nazo wafanyabiashara ikiwemo changamoto ya tozo ambazo ni
kero.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mnada huo Bw.Kerambo Samweli amesema mwaka jana
waliweza kukusanya mapato na kupitiliza malengo lakini kwasasa wanaona
haitawezekana kutokana na kupungua kwa uingiaji wa mifugo kwenye mnada
huo kwa mwaka huu.
“Tulifanikiwa
kukusanya zaidi ya malengo kwa mwaka 2018/2019 tulikusanya kwa 112% pia
kwa mwaka wa 2019/2020 tumefanikiwa kukusanya kwa 88.8%”. Amesema
Bw.Kerambo.