Vigogo wengine 6 wa jeshi la zimamoto wawasili takukuru makao makuu dodoma kuhojiwa

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waliokuwa
wajumbe wa kamati ya utekelezaji  wa makubaliano  iliyosainiwa tarehe
22,Agosti ,2019  kati ya jeshi la zimamoto na uokoaji  na kampuni ya ROM
Solutions  Co.LTD leo Feb.5,2020 wamewasili ofisi za  Taasisi ya kuzuia
na kupambana na Rushwa [TAKUKURU]makao makuu jijini Dodoma kwa ajili ya
kuhojiwa kutokana na kashfa ya kufanya mkataba mbovu wa Trilioni Moja
bila kupitishwa na  bunge.

Idadi
ya  wajumbe waliofika katika ofisi hizo leo  ni sita ambapo walifika 
ofisi za TAKUKURU pamoja na kompyuta mpakato [Laptop]walizopewa na
kampuni ya ROM SOLUTIONS CO.LTD.

Wajumbe
hao pia walikuwa wakilipwa posho za vikao USD 800   na kampuni hiyo 
wakati wakiwa wanakutana katika vikao vyao  vya majadiliano.

Wajumbe
hao ni pamoja na Kamishna wa zimamoto  Mbaraka Semwanza,Naibu Kamishna 
wa zimamoto Fikiri Salla,Naibu Kamishna wa Zimamoto  Lusekelo Chaula’.

Wengine
ni Naibu Kamishna  zimamoto Ully Mburuko,Mchumi zimamoto Boniface
Kipomela  na Mchumi  wa jeshi hilo la zimamoto na uokoaji Felis Mshana.

Ikumbukwe
kuwa sakata hilo  la mkataba mbovu  wa Trilioni moja limesababisha
aliyekuwa waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola kuachishwa
wadhifa huo na kuteuliwa mwingine  hivi karibu George Simbachawene.