Mtafiti
wa mradi wa Utafiti wa sera za kilimo Afrika (APRA) Prof.Ntengua Mdoe
akifafanua kuhusu kilimo biashara cha mpunga, mifugo na hali maisha ya
wakulima wadogo katika bonde la Kilombero katika semina ya waandishi wa
habari iliyofanyika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Mkoani Morogoro.
*******************************
Watafiti
wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA katika Utafiti wao wamebaini
kuwa Vijana hasa wa kiume ndio wanaonufaika zaidi ni Kilimo biashara cha
Mpunga kwenye bonde la Kilombero ijapokuwa wanachangamoto ya mitaji na
kukosa mashamba binafsi.
Hayo
yamebainishwa na Prof. Ntengua Mdoe wakati akiwasilisha mada ya utafiti
wake kwa Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye
warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Mradi wa utafiti wa Sera za Kilimo
barani afrika APRA iliyolenga kutoa matokea ya utafiti wao kwa jamii
kupitia vyombo vya habari.
Akiwasilisha
matokeo ya Utafiti wake uliohusu ushiriki wa vijana kwenye Kilimo
biashara cha Mpunga kwenye bonde la Kilombero Prof. Mdoe amesema vijana
wenye umri kati ya miaka 15-35 ni ambao ni sawa na asilimia 35.5% ya
watu ndio wenye kunufaika zaidi katika bonde hilo ukilinganisha Makundi
mengine.
Amefafanua
kuwa kwenye utafiti wao huo wamebaini kuwa sio kweli kwamba vijana
hawashiriki kwenye shighuli za kilimo bali wanashiriki vizuri kwenye
Kilimo biashara cha Mpunga pamoja na kwenye mnyororo mzima wa thamani wa
zao hilo katika maeneo mbalimbali.
Amesema
kwenye Utafiti huo umebaini kuwa kipato wanachokioata vijana kwenye
nguvu wanayowekeza kwenye Kilimo ni kikubwa kuliko nguvu inayowekezwa na
vijana wanaofanya kazi zingine hapa nchini.
“Ukiangalia
kwenye Utafiti tumebaini kuwa nyumba nyingi zinazoongozwa na vijana
zina uhakika mkubwa wa chakula kuliko kaya ambazo zinaongozwa na wazee
na watu Wenye umri Mkubwa na hii ni kutokana na mafanikio makubwa
wanayoyapata kutoka kwenye Kilimo” Alisema Prof.Mdoe.
Katika
mapendekezo ya ya utafiti huo Utafiti huo umetaka Halmashauri na
Serikali za mitaa kutenga Ardhi ya Kilimo kwaajili ya vijana kama
ambavyo imeelekezwa kwenye sheria ya Ardhi ya Mwaka 1999 lakini pia
kuwasaidia mikopo kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana wa asilimia 4%
kwenye mapato ya Halmashauri.
“Tunashauri
pia Halmashauri za Wilaya kwa kushirikiana na wadau wengine wa Kilimo
kuwawezesha vijana kupata elimu ya Kilimo Bora kupitia mafunzo ili
kuongeza tija zaidi na kuachana na Kilimo cha mazoea” Alisema Prof.
Mdoe.
Akitoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali ya Wanahabari hao Mkuu wa Mradi
huo wa APRA upande wa Tanzania Prof. Aida Isinika amesema vijana wengi
wanapenda Kilimo chenye tija na soko zaidi kama vile Mpunga, Vitunguu,
Nyanya na mazao mengine.
“
Vijana hawataki mazao ya muda mrefu maana sio wavumilivu saa wanahitaji
matokeo ya muda mfupi ndio maana unaona wengi wanakimbilia mazao hayo
ambayo wanatumia muda mfupi kupata fedha” Alibainisha Prof. Isinika.
Prof.
Isinika amesema mitaji wanayohitaji vijana ni midogomidogo na sio
mikubwa sana hivyo wakiwezeshwa kupata itawasaidia sana katika kufanya
shighuli za Kilimo kwa urahisi na kuongeza tija huku wakibiresha maisha
yao.