Viongozi wa wizara ya fedha na mipango, nishati na tanesco waridhishwa na mradi wa backbone zuzu jijini dodoma

 


Viongozi wa Wizara ya Fedha na
Mipango,Nishati pamoja na TANESCO wakimsikiliza  Mratibu wa Mradi wa
kituo cha kupoza umeme Zuzu, Mhandisi Peter Kigadye walipotembelea na
kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu leo Julai 26,2021
kilichopo jijini Dodoma.



Viongozi wa Wizara ya Fedha na
Mipango,Nishati pamoja na TANESCO wakimsikiliza  Mhandisi wa Kituo cha
Zuzu Nzingula Sospeter walipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha
kupoza umeme cha Zuzu leo Julai 26,2021 kilichopo jijini Dodoma.



Baadhi ya Mitambo inayofanya kazi katika  kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.



Viongozi wa Wizara ya Fedha na
Mipango,Nishati pamoja na TANESCO wakiendelea na ziara ya kutembelea  na
kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu leo Julai 26,2021
kilichopo jijini Dodoma.


Na Alex Sonna,Dodoma


Viongozi wa Wizara ya Fedha na
Mipango,Nishati pamoja na TANESCO wameridhishwa na utekelezaji wa mradi
wa ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha Umeme (Backbone) awamu ya pili
kituo cha Zuzu Jijini Dodoma.


Akizungumza leo
Julai 26,2021,wakati wa ziara ya kukagua kituo hicho cha kupooza umeme
kilichopo Zuzu Jijini Dodoma, Kamishna  wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya
Fedha na Mipango, Sauda Msemo ambaye alimwakilisha Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo amesema wameridhishwa na jinsi ambavyo mradi huo
unatekelezwa.


“ Sisi
tumeridhishwa na utekelezaji ikiwa na mikakati mbalimbali ambayo
imefikiwa ya kuhakikisha miradi inafikiwa, tunaendelea kushirikiana
vizuri sisi Wizara ya Fedha na Mipango na wenzatu wa Wizara ya Nishati
na Tanesco ili kuhakikisha tunafikia malengo kwa mafanikio makubwa,”
amesema


Amesema wamefika
katika kituo hicho  ili kuona hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa
mradi na kuwa na uwezo wa kupokea umeme wa kiwango kinachotakiwa


“Huu
ni  mwendelezo wa ziara tulianzia katika Bwawa la Mwalimu Nyerere
tukafuatiwa na Kinyerezi kisha Chalinze kuona zile substation (vituo vya
umeme) kwa hiyo nimwendelezo ilikuwa na lengo la kuona miradi hii na
hatua ambazo zimechukuliwa,”amesema.


Amesema Wizara ya
Fedha na Mipango itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali
ambayo ina manufaa kwa nchi huku ikiendelea kusisitiza umuhimu wa
ushirikiano ili kutekeleza miraji yenye tija.


“ Tumekuwa
tukitoa fedha vizuri na kwa wakati sisi tunaendelea kushirkiana kwa
karibu kwa sababu tunaelewa umuhimu wa miradi hii kwa hiyo Wizara ya
Fedha na Mipango inaendelea kusisitizia suala la ushirikiano na chochote
kinachotokea ili kuwe na uelewa wa pamoja,”amesema.


Kwa upande wake,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali amesema
wamekamilisha ziara ya kukagua kituo hicho cha kufufua umeme na
wamefarijika kwa viongozi hao kufika katika kituo hicho.


“ Tumekamilisha
ile ziara ambayo tumeanza nayo ambapo wameangalia tutakavyoutoa umeme
kutoka Julius Nyerere mpaka chalinze na kutoka Chalinze mpaka Dodona,
kwa ujumla sisi tumefarijika kuwapata viongozi kuja kutembelea ni wadau
muhimu kwetu.


“ Tumepata fursa
ya kuweza kujadiliana na kuwa na uelewa wa pamoja na tunatumai baada ya
ziara hii itasaidia zaidi katika majukumu yao katika sekta ya
nishati,”amesema.


Kwa upande wake,
Mhandisi Mkuu kutoka Shirika la Umeme Tanzania Dodoma, Donasiano Shamba
amesema wamenufaika na mradi huo kwani Megawati zimeweza kuongezeka.


“Sisi kama
watumiaji Mkoa wa Dodoma tumenufaika sana na mradi huu  huko nyuma
tulikuwa na Megawati 34 ina maana  transfoma zilizokuwepo zilikuwa ni
mbili ambazo   Capacity  yake ilikuwa jumla ni Megawati 32 lakini baada
ya mradi huu ambao umeongeza transfoma 2 kila moja ilikuwa na uwezo
megawati 100 hivyo tumekuwa na megawati 200,”amesema.


Amesema miaka ya
nyuma umeme wa Mkoa wa Dodoma haukuwa katika hali nzuri  lakini baada ya
kuongeza transfoma umeme umekuwa vizuri.


“ Mwaka 2015
tulikuwa na wateja wachache lakini baada ya Serikali kuhamia Dodoma
wananchi wameongezeka sana  sasa hivi tuna wateja zaidi ya
160,000  kwahiyo hiyo yote sababu ya uwepo wa kituo hiki inatupa uwezo
wa kuendela kuwahudumia wananchi,”amesema.


Naye Mratibu wa
Mradi wa kituo cha kupoza umeme Zuzu, Mhandisi Peter Kigadye, amesema
kuwa ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha Umeme (Backbone) awamu ya pili,
gharama za mradi huo ni Dola milioni 54.3 pamoja na kituo  cha Mkoani
Singida.


Mhadisi Kigadye amesema mradi kama huo unatakelezwa katika vituo vinne vya  Iringa, Shinyanga, Singida, Iringa na Dodoma.


Akikizungumzia
kituo cha Zuzu, kigadye amesema ni  muhimu kwani  kitapokea umeme kutoka
katika Bwawa la Mwalimu  Julius Nyerere na kupeleka maeneo ya Kaskazini
mwa Nchi  kupitia Singida na maeneo ya Kusini kupitia Iringa.


Amesema kituo
hichi kinatarajia kukamilika Septemba mwaka huu huku akidai changamoto
waliyokutana nayo ni katika  uingizaji wa vifaa kutokana na kuzuiliwa
kwa safari kwa sababu ya janga la ugonjwa wa Corona.