Wakulima morogoro wanufaika na mradi wa kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga

 

Picha ikionesha Mfereji mkuu unaoepeleka maji mashambani katika skimu ya Msolwa Ujamaa.

Bi Wadara Kitada Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Mlimba Mkoani
Morogoro akizungumza katika skimu ya Njage wakati wa ziara ya kikazi
katika miradi ya kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga.
Picha Ikionesha Ghala la kuifadhia mazao katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Njage katika Halmashauri ya Mlimba

Sehemu ya Miundombinu katika skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji Msolwa ujamaa Kilosa mkoani Morogoro.

NA; MWANDISHI WETU – MOROGORO

Wakulima
katika skimu za kilimo cha umwagiliajiMvumi, Msolwa Ujamaa na Njage
zilizopo katika Wilaya ya Kilosa, Kilombero na Halmashauri ya Mlimba
Mkoani Morogoro,zimenufaika na ukamilishwaji wa ujenzi wa skimu za
kilimo cha umwagiliajizilizopochiniyamradiwakuongezauzalishajiwazao la
mpungauliyofadhiliwanaBankyaDunia.

Wakiongea katika nyakati
tofauti baadhi ya wakulima katika skimu hizo, walisema hali ya kilimo
katika skimu hizo haikuwa rafiki kabla ya kuwepo kwa ujenzi wa
miundombinu hiyo ambapo kwasasa, hali ya kilimo ni nzuri kwani kuna
uhakika wakupata wastani wa mavuno ya gunia 20 mpaka 30 kwa heka
kutokana na uhakika na matumizi sahihi ya maji katika misimu tofauti ya
kilimo.

Bi Mwanaisha Kaluwa mkulima katika Skimu ya Mvumi
Wilayani kilosa amesema “Naishukuru Serikali kwa kushirikiana na Benki
ya Dunia kwa kutuletea mradi wenye manufaa kwetu sisi wakulima lakini
Ombi langu ni kwamba Serikali itutafutie masoko ya uhakika kwani kwa
sasa tunauza kupitia madalali ambao wanatuumiza sana ,hawatumii
vifungashio halali wanafunga kwa kutumia rumbesa, tunaomba sana Serikali
isimamie mpunga uuzwe kwa kutumia mizani.” Alisema Bi. Mwanaisha.

Afisa
kilimo wa Halmashauri ya Mlimba Bi WadaraKidata,akizungumzia skimu ya
kilimo cha umwagiliaji Njage alisema kabla ya mradi skimu ilikuwana
changamoto ya maji ambayo kwa sasa wanapata maji kwa wakati barabarani
nzuri ambazo zinarahisisha mazao kufika ghalani na kwa wanunuzi kwa
wakati na gharama nafuu.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mhandisi
wa mkoa wa Umwagiliaji Morogoro Njanji Mlole,alisema kabla ya kukabidhi
mradi huo ambao upo katika muda wam atazamio, mapungufu machache
yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na kurekebisha mabanio na kuinua sehemu
ya vipange vya barabara za skimu na kubadilisha ma karavati katika skimu
ya Njage Mlimba,pamoja na kuingiza mfumo wa majisafi katika vyoo
yatarekebishwa katika kipindi hicho kwa mujibu wa mkataba.