Walaji nguruwe hatarini kupata kifafa , ni ugonjwa unaoenezwa na minyoo ya tegu inayopatikana kwa wingi katika nyama ya nguruwe

picha ikionyesha  Naibu Wa  afya Faustin Ndugulile wa kwanza
kushoto katikati ni mkuregenzi mkuu wa Taasisi ya magonjwa ya binadamu (NIMR)Prof  Yunus
Mgaya wakifatilia  mada zilizokuwa zikiendeshwa katika mkutano za
namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Tegu la nguruwe
Pprof  Helene Carabin kutoka nchini Canada akitoa
 
mada katika  mkutano huo
Na Woinde Shizza ,Arusha



Minyoo  ya Tegu ya Nguruwe (cysticercodis)imekuwa tishio kwa walaji wa nyama ya mnyama huyo  na kupelekea kusababisha maradhi mengi kwa binadamu ikiwemo ugonjwa Wa kifafa.




Hayo yamebainishwa na Naibu Wa  afya Dkt. Faustin Ndugulile wakati akifungua mkutano  Wa kwanza Wa  kimataifa Wa kujadili minyoo ya Tegu Wa nguruwe katika thana ya Afya ya pamoja unaofanyika katika ukumbi Wa Mounti  Meru Arusha






Mkutano huo umefanyika Leo November 26 ambapo alisema kuwa kwa wale walaji Wa Nyama ya Nguruwe kunaminyoo ambayo iko  katika nyama huyo kupitia mayai yanayopatikana  ndani ya  inaweza kumuathiri binadamu endapo atakula nyama ambayo ijapikwa vizuri pamoja na   mbogamboga ambazo azijaoshwa  pamoja nakupikwa vizuri.






Alisema athari zinazoweza kupatikana katika mnyama huyu ni kubwa ikiwemo kupata ugonjwa Wa kifafa , na tatizo hili limeshaingia katika nchi yetu na limeanza kuathiri zaidi katika mikoa ya  Manyara, Njombe,   Mbeya ,Sogwe ,Mbeya pamoja na mkoa Wa Arusha na asilimia 16%ya wananchi wanaoishi mikoa hii wameshaathirika na ugonjwa huu.






 “Lengo kubwa kuweka mkakati Wa pamoja Wa jinsi gani tunaweza kutokomeza ugonjwa huu Wa minyoo Wa Tegu Wa Nguruwe,nanianze kutoa rai kwa wafugaji Wa Nguruwe kufuga kisasa na kuacha wanyama wao kuzurura hovyohovyo kwani anavyozurura ovyo anaeza kuacha kinyesi chenye mdudu huyo katika mboga.
  na pia wapate ushauri sahii wawataalamu Wa mifugo Wa namna ya kufuga mnyama huyo ,pia wale wachinjaji Wasifanye uchinjaji Wa mnyama huyu bila kizingatia utaalamu na msingi wawataalam wanaosimamia wanyama hao,aidha pia nitoe rai kwa wale wanaokula mnyama huyu kuhakikisha kwamba kimepikwa vizuri na sio mnakula nyama yenye damu damu yaani ile mbichimbichi kwani inaweza  kukuletea mathara
” alisema


 Alibainisha kuwa hadi sasa serikali yetu haijapata chanjo kwa ajili ya kumzuia mnyoo huyo wa nguruwe na ipo katika utafiti wakuangalia namna ya kumthibiti,lakini pia tunaweza kuzuia  kwa kuakikisha kuwa tunafuga bila mifugo yetu kuzagaa,pia kwa wale tunaochinja tuhakikishe tumewapima mifugo yetu kwanza bila ya kuwachinja



Kwa upande wake mkuregenzi mkuu wa Taasisi ya magonjwa ya binadamu (NIMR)Prof  Yunus Mgaya wanatekeleza mradi huu kwa kusanya taarifa za kutosha kuhusiana na minyoo huyu wa Tegu ambaye anapatikana kwa kula mbogomboga ambazo zimebeba mayai yaliotokana na vinyesi vya nguruwe au kinyesi cha binadamu


“mradi huu unatekelezwa na nchi zingine mbili Afrika ambazo ni Msumbiji pamoja Zambia  na tunashirikiana na wadau wetu wa utafiti wa ujerumani kutoka chuo kikuu cha  Munchen  ,mradi huu umetuwezesha kununua vifaa vya maabara kwa ajili ya kuweza kufanya utafiti wetu vizuri kwa kiwangoncha juu ,pia umetusaidia kuwapeleka vijana wetu kwenda kupata elimu  katika shahada zauthamini PHD, lakini mradi huu umetuleta pamoja nchi hizi za Afrika  na lengo kubwa ikiwa  ni kutokomeza au kuzuia watu wasipate ugonjwa huu unaotokana na minyoo hii ya Tegu ”



Naye Kaimu mkuu wa idara ya tiba ya mifugo na afya ya jamii ambaye  pia ni mkurugenzi wa mtandao wa utafiti wa kisayansi  Prof,Helena Ngowi  alisema kuwa mnyoo ni hatari sana kwa sababu anaweza kuleta adhari kubwa katika utumbo wa binadamu hadi katika ubongo wa binadamu.

Asema anaamini bila ya kuwa na mfugo alie athirika binadamu hawezi kupata ugonjwa huo na kwamba tafiti hizo zilianza kufanyika tangu mwaka 199 na bado zinaendelea  na kiwango cha tatizo kimeshajulikana ,tunashirikiana kwa lengo la kushirikiana katika kupambana na tatizo hili kwa sababu hazina mipaka ,kwa ivyo tunavyoshirikiana na nchi hizi zingine  tunaweza kutokomeza kabisa tatizo hili pia tutashirikisha jamii ili tuweze kutokomeza .