Wananchi arusha wapuuza matumizi ya vifaa vya kujikinga na corona

Na Claud Gwandu, Arusha  

LICHA ya Serikali
kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga na maaambukizi
ya virusi vya corona bado baadhi ya wananchi Jiji la Arusha wamekuwa wakipuuza
zoezi hilo.

 

Wakizungumza na blog hii baadhi ya wananchi katika
jiji la Arusha wamesema kuwa jamii imekuwa ikipuuza uvaaji sahihi wa vifaa vya
kujikinga na corona   ikiwemo kuvaa barakoa kwa siku tatu bila kuifua
jambo linaloweza kuhatarisha maambukizi mapya.

 

Wananchi
hao walisema kuwa wanapaswa kuendelea kutumia vizuri vifaa hivyo vya kujikinga
dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Corona ili kuweza kuweka jamii katika sehemu
salama zaidi.

 

“Wananchi
wengi hivi sasa wameacha kunawa mikono au kutakasa mikono yao Kutokana na
kuamini kuwa ugonjwa huo umeisha jambo ambalo sio sahihi kutokana na Corona
kuwepo kwenye nchi za jirani jambo ambalo linasisitizwa na serikali kuendelea
kujinga na Corona”walisema

 

Walisema baadhi
ya wananchi wamekuwa wakivaa barakoa zaidi ya masaa matatu au wakivaa barakoa
hizo tofauti na maelekezo sahihi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Corona 
kama
yanavyoelekezwa na taasisi za afya.

 

Paul
Loishiye anayejitambulisha kama mdau wa masuala ya Afya  mkoani Arusha alisema
kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kusikiliza vyombo mbalimbali vya habari ili
kujua nini kinaendelea na kupata elimu ya virusi vya Corona kutoka katika taasisi
za kiserikali na taasisi nyingine. 

 

Naye Dkt. Innocent
Lyamuya mdau wa masuala ya Afya mkoani Arusha  aliishauri jamii kuendelea kufuata ushauri
uliowekwa na wataalamu wa afya ikiwemo kutumia barakoa kwa usahihi pamoja na
kutumia vitakasa mikono ili kujikinga na corona.

 

Dkt Lyamuya
ambaye ni mfanyakazi katika hospitali ya rufaa ya ALMC Jijini Arusha amesema wamekuwa
wakitoa elimu kwa wananchi ya kujikinga na Corona huku akiwataka wananchi
kuendelea kuzingatia usafi.

 

“Sisi ukija hospitalini
lazima uvae barakoa kwaajili ya kujikinga na maradhi ya corona, ijapokuwa
Tanzania ugonjwa umeisha lakini ni lazima watu wajikinge na wafanye kuvaa vifaa
hivyo ni kama utamaduni, huwezi kujua ugonjwa utaibuka lini tena,”alisema.

 

Alisema
kuwa wananchi wanatakiwa kuendelea kuzingatia kufanya usafi na kuwa wasafi muda
wote  na kwamba hiyo ndio njia sahihi
kuepukana na maambukizi ya virusi vya Corona. 

 

David
alisema wamekua wakitoa elimu mara kwa mara kwa viongozi mbalimbali juu ya
kujikinga dhidi ya virusi vya Corona hasa katika yote ya umma 

 

Serikali kupitia
Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto imesema kuwa ili
kukabiliana na maambukizi ya Corona ni vyema wananchi wakaepukana na
mikusanyiko isiyokuwa na lazima, kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji Tiririka
na sabuni pamoja na kutumia vitakasa mikono.