Wakazi, wa Kata za
Ndala, Masekelo na Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga wameiomba serikali kukamilisha
ujenzi wa Barabara kipande cha kuelekea katika hospital ya rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga ili kuwaepusha na athari ya vumbi kali linalotimuka.
Kwa nyakati tofauti
wamezungumza watumiaji wa Barabara hiyo, madereva wa magari,Bajaji, waendesha
Baiskeli, pikipiki pamoja na wananchi wanaoishi kando kando ya Barabara hiyo
kipande cha kata za Ndala,Masekelo,na Mwawaza ambao wamelalamikia vumbi kali
linalotimuka na kutishia usalama wa afya zao
Wameiomba serikali kutimiza
ahadi yake ya kukamilisha ujenzi wa Barabara hiyo kwa kiwango cha lami ili kuwaepusha
na madhara ya kiafya yanayoweza kusababishwa na Vumbi kali linalotimuka mchana
na usiku
Meneja wa Wakala wa
Barabara Mijini na Vijijini TARURA Wilaya ya Shinyanga, Injinia Samson Pamphil amesema Barabara hiyo
ipo kwenye mpango wa ukamilishaji kwa kiwango
cha lami kama ilivyoahidiwa na serikali ambapo amewaomba wananchi kuwa na subira kwani
kinachosubiriwa ni fedha kutoka serikali kuu.