Afisa wanyamapori mkuu kutoka
Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Antonia Raphael akitoa ufafanuzi kwa
wanawake kuhusu utaratibu wa malipo ya kifuta machozi kwa wakazi wa
kijiji cha mheza wilayani same, mkoani Kilimanjaro.
Washiriki wa mafunzo wakichanganya
pilipili na mchanga ili kutengeneza vilipuzi salama kwa kufukuza Tembo
Shambani kwenye mafunzo ya mbinu za kudhibiti migongano baina ya
wanyamapori wakali na waharibifu katika kijiji cha Muheza wilaya ya Same
mkoani Kilimanjaro.
Washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye
mafunzo ya ujenzi wa uzio wa kudhibiti Tembo kuingia Shambani na
kuharibu mazao kwenye mafunzo ya mbinu za kudhibiti migongano baina ya
wanyamapori wakali na waharibifu kwenye kijiji cha Muheza ,wilaya ya
Same mkoani Kilimanjaro
Washiriki wa mafunzo wakipatiwa
elimu ya uwekaji wa mizinga ya nyuki kando ya shamba kwa ajili ya
kulinda mazao dhidi ya Tembo kwenye mafunzo ya mbinu za kudhibiti
migongano baina ya wanyamapori wakali na waharibifu aliyofanyika kwenye
Kijiji cha Muheza, wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Wizara ya Maliasili na Utalii
imewataka wananchi wa Kata ya Maore wilayani Same mkoani Kilimanjaro
kutumia kwa usahihi mafunzo ya kujikinga na wanyamapori ili waweze
kuyalinda mazao yao bila ya kusababisha madhara kwa wanyamapori.
Akizungumza na wananchi Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) Dkt. Emmanuel Masenga
amesema endapo wananchi watayatumia vema mafunzo hayo watapunguza kwa
kiasi kikubwa ugumu wa kazi ya kufukuza Tembo mashambani.
Aidha, Dkt. Masenga amewakumbusha wananchi kuepuka kufanya
shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo kwenye maeneo ya jirani na
hifadhi.
Kwa upande wake, afisa wanyamapori
mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii , Bi. Antonia Raphael amesema
mafunzo hayo yatakuwa endelevu katika maeneo mengine lakini pia wizara
imeweka Utaratibu mzuri wa ufuatiliaji wa wale wote waliopata mafunzo
hayo ili kuona kama wanatekeleza kile walichojifunza.
Mafunzo hayo kwa vitendo yalihitimishwa leo kwa wananchi wa Same na baadae washiriki waliofuzu walipatiwa vyeti.