Wanawake hanang’ wanufaika na mradi wa kilimo kutoka shirika la oxfam & ucrt

Felista Giyam mhasibu wa kikundi cha hamasa ameiomba
serikali kuona uwezekano wa kutafuta masoko kwa mazao ya wakulima kwani
wamekuwa wakilima kwa muda mrefu lakini wanakosa masoko hivyo
kuwakatisha tamaa licha ya kukiri kuwa wamekuwa na faida kwa wastani
japo soko linaendelea kuwa kikwazo licha ya kwamba pia wakulima wamekuwa
wakitumia gharama kubwa katika pembejeo za kilimo
Anna Iselu mbaye ni mhasibu wa kikundi cha wanawake na vijana cha Gosanga anasema mradi huo  utawafanya
kutokuonekana mizigo ndani ya familia na kwa jamii kwa ujumla na kuleta
mtazamo mwingine mpya na chanya miongoni mwa jamii
Albert
Masuja muwakilishi kutoka shirika la UCRT wamewawezesha jumla ya
wanawake 45 katika Kijiji Mureru kata ya Balangdalalu wilayani hanang
kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji ili kuondokana na utegemezi wa
asilimia 100 kwa wanaume zao.
Baadhi ya wakinanana wanufaika wa mradi huo wakibadilishana mawazo wakiwa sahambani kukagua mazao yanaendeleaje 
Donath Fungu Meneja wa miradi ya  Oxfam kanda ya kaskazini akitoa ufafafanuzi wa mradi huo unavyoendelea kwa sasa 
 Charles Kidaguwi mmoja
wa wanaume walioshiriki katika mradi huo wa wanawake na vijana kwaajili
ya kujikwamua kiuchumi katika kijiji cha Mureru wilayani Hanang’  mkoa
wa Manyara.
  Anna Iselu mbaye ni mhasibu wa kikundi cha wanawake na vijana cha Gosanga akikagua mazao katika shamba la mradi wa wanawake na baadhi ya wanaume waliojiunga katika vikundi hivyo

Charles Kidaguwi ambaye ni mmoja wa wanakikundi na mlizi wa shamba la mradi akifurahia jambo 
Baadhi
ya wanakikundi wakitoka kukagua shamba la mradi wa mahidi waliowezeshwa
na Oxfam pamoja na  Acrt amabao wanatarajia kuvuna zaidi ya magunia
100-150 kwa mujibu wa wataalam wa kilimo.
Na Vero Ignatus,Manyara.

Katika
kuhakikisha kuwa jamii inajikwamua kiuchumi shirika la Oxfam Tanzania
kwa kushirikiana na Ujamaa community resources (UCRT wamewawezesha jumla
ya wanawake 45 katika Kijiji Mureru kata ya Balangdalalu wilayani
hanang kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji ili kuondokana na
utegemezi wa asilimia 100 kwa wanaume zao.

Wakieleza
manufaa ya mradi huo kwao wanawake hao kwa nyakati tofauti wamesemakuwa
mradi huo utawafanya kutokuonekana mizigo ndani ya familia na kwa jamii
kwa ujumla na kuleta mtazamo mwingine mpya na chanya miongoni mwa jamii
wilayani hapo kufuatia jamii ziishio Hanang kutokumpa nafasi mwanamke
hivyo kuendelea kuwa na uchumi tegemezi kwa miongo yote.

“Huu
mradi kwakweli kwanza tunawashukuru Oxfam na Ucrt kwa kutuletea mradi
huu unajua huu mradi utatukwamua sana kiuchumi na hata kusaidia baadhi
ya majukum kwenye Familia”alisema Felista Giyam ambaye ni mhasibu wa kikundi cha wanawake hao
.

 Ameongeza
kuwa pamoja na mradi huu kulenga wanawake ndani yake kuna wanaume ambao
tumeamua kushirikiana nao kwani sisi tunaamini 
“hapa ndani ya mradi kuna wanaume 12 kati yet una hapo tumeamua sana katika umoja.kushirikiana kwa sababu ni mwanzo” Alisema Felista

Mmoja ya wanakikundi mwingine Anna Iselu pia
kwa niaba ya wanawake hao na kikundi hicho cha muungano ameiomba
serikali kuona uwezekano wa kutafuta masoko kwa mazao ya wakulima kwani
wamekuwa wakilima kwa muda mrefu lakini wanakosa masoko hivyo
kuwakatisha tamaa licha ya kukiri kuwa wamekuwa na faida kwa wastani
japo soko linaendelea kuwa kikwazo licha ya kwamba pia wakulima wamekuwa
wakitumia gharama kubwa katika pembejeo za kilimo.

 “Unajua
hapa tunatumia gharama kubwa wakati wa kununua pembejeo lakini tunakosa
masoko jambo hili linaturudisha nyuma kwakweli serikali iangalie namna
ya kuwawezesha wakulima hasa sisi wanawake ambao tumeamua kujiingiza
katika kilimo
” Alisema Anna Iselu mmoja ya wanakikundi.

Charles Kidaguwi ni
kati ya wanaume ambao wameshiriki katika mradi huo amesema kwake una
manufaa makubwa kwani utamsaidia kuwajibika vyema katika familia zaidi
tofauti na awali kwani kwake  ni  chanzo kimojawapo cha mapatao ,pia kwa
upande wa mwanamke itamsaidia kujikwamua kiuchumi,na kutoa mchango
katika familia tofauti na awali walikuwa wanakaa nyumbani pekee.

Kwasababu
sikuzote familia inalaliaga upande wangu lakini kama mama amepata mradi
huu wa kilimo basi na mimi nitapata msaada mkubwa alisema Chalrles
Kidaguwi kutoka Kijiji cha Mureru wilaya ya Hanang’ mkoa wa Manyara

Kwa upande wake Donath Fungu Meneja
wa miradi ya  Oxfam kanda ya kaskazini amesema mradi huo wanaufanya kwa
kuwashirikisha wanawake na vijana lengo likiwa ni kuwajengea  wanawake
uwezo kiuchumi kipato kiuchumi kwani mwanamke anajishughulisha na mambo
mengi ila jamii haimtambui

Ukimuwezesha
mwanamke umeiwezesha familia ,jamii na Taifa kwa ujumla hivyo Oxfam
Tanzania nzima mdau wetu mkubwa tunaesgughulika nae ni mwananmke,kitendo
chake cha kutambulika  kinatokana na nguvu yake ya kiuchumi kuwa ndogo
tunaamini kwamba atakapopata nafasi ya kuinuka kiuchumi

Fungu
amesema mwanamke atakapopata nguvu ya kuinuka kiuchumi atapata nafasi
ya kufanya maamuzi katika ngazi ya kifamilia Kijiji hadi ngazi ya
kitaifa,amesema pamoja na hayo pia wanawapatia mafunzo ya uongozi
,kujiamini ambapo hadi sasa wamefikia hatua kubwa 

Amesema
hapo awali katika wilaya hiyo mwanamke alikuwa haruhusiwi kusimamam
mbele ya jamii na kuzungumza chochote ila baada ya mafunzo waliyowapatia
wameweza kujiamini na  baadhi yao wameweza kugombea nafasi mbalimbali
katika ngazi za vijiji,kuwepokatika na kamati za vijiji na nafasi
mbalimbali muhimu.

Naye
Mratibu wa Mradi kutoka  UCRT Masuja alisema kuwa malengo ni kumpa
mwanamke fursa ili aweze kuboresha Maisha yake kiuchumi ambapo wameweza
kuwaweka katika vikundi ili waweze kufanya kazi kwa pamoja na kuleta
ufanisi Zaidi

Amesema
katika kushirikiana na Oxfam wameweza kutoa nafasi kwa mwanamke
kumiliki ardhi wapatao 365 pamoja na kuwapatia hati miliki,pia wameweza
kuwapatia wakinamama wa kikundi cha hamasa ng’ombe wapatao 9 na sasa
wamepo 18 lengo ni kuwakwamua kiuchumi pamoja na vijana kujitambua na
kujiandaa kuja kuwa na familia baada
e.