Watoto chini ya miaka 5 kupata cheti cha kuzaliwa bure


Na.Farida Saidy,Morogoro



Wakala Wa Usajili Ufilisi Na
Udhamini (RITA) Kupitia Wasajili Wa Huduma Ya Uandikishaji Watoto Chini
Ya Umri Wa Miaka Mitano Wametakiwa  Kutofanya Urasimu wa kuwatoza  Watu
Fedha kwa ajiri ya malipo ya ya cheti cha kuzaliwa,  Ikiwa Mkakati
Uliopo sasa Ni Kusajiliwa Bure, Na Kwa Atakaebainika Kufanya Hivyo Hatua
Kali za kisheria Zitachukuliwa Dhidi Yake.


Kauli Hiyo Imetolewa Na Mkuu Wa
Mkoa Wa Mororgoro Bw.Loata Ole Sanare Wakati Wa Ufunguzi Wa Semina
Ya  Wakala Wa  Usajili Ufilisi Na Udhamini  (RITA)  Uliowahusisha
Viongozi Mbalimbali Wa Kimkoa Wenye Dira Ya Kufikia Lengo La Kusajili
Watoto Zaidi Y Asilimia 90 Ya Watoto Wote  Bure , Wenye Umri Chini Ya
Miaka Mitano Mkoani Morogoro.


Kwa Upande Wake Kaimu Afisa
Mtendaji Mkuu  Kutoka RITA Bi.  Emmy Hudson  Amesema Ili Kukamilisha
Majukumu Kwa Watendaji Kuhusu Mpango Huo,Wameandaa Mafunzo Kwa Wahusika
Wote ,Wakiwemo Watumishi Sita Kutoka Kila Halmashauri  Mkoani  Morogoro
,Pamoja Na Mtumishi Mmoja Mmoja Kutoka Idara Ya Usalama Na Idara Ya
Uhamiaji .


Nao Baadhi Ya Washiriki Wa Semina
Hiyo Wakiwemo Viongozi Mbalimbali Wa Kiserikali Na Kidini Wameusifu
Mpango Huo Wa  Usajili  Bure Wa Watoto Wenye Umri  Chini Ya Miaka Mitano
Unaoendelea Kuifikia Mikoa Mbali Mbali Nchini Na Kusema Kuwa
Utawasaidia Katika Kuharakisha Upatikanaji Wa Haraka Wa Vyeti Hivyo.


Ikumbukwe Kuwa  Kundi La Awali La
Watoto  Walio Chini Ya Umri Wa Miaka Mitano Limekwishaanza  Utekelezaji
Wake Ambapo Ni Mikoa Ya Mbeya  Songwe Mwanza Njombe
Iringa  Geita  Shinyanga Lindi Mtwara Mara Simiyu Dodoma Na Singida
Ambapo Kwa Sasa Ni Zamu Ya Morogoro Pamoja Na Pwani.