Na Daud Tiganya
SERIKALI Mkoani Tabora imewakabidhi watoto wawili waliokuwa wamepotea mkoani Mbeya kwa wazazi wao wakiwa na afya njema.
Hatua
hiyo inatokana na kupatikana mmoja wao akiwa na mama mmoja Hawa Ally
katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega baada ya wasamaria wema kuwa na
wasiwasi na mtuhumiwa na kutoa taarifa Polisi.

Akikabidhi
watoto hao leo Mkuu wa Mkoa wa Tabora ametoa onyo kwa wale wote
wanaohusika na vitendo vya aina hiyo ikiwemo kuiba watoto wachanga na
kwamba Serikali itahakikisha inawachulia hatua kali za kisheria.

Aliwataka
wito kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao badala ya kuwategemea
wasaidizi wa kazi ndio watumike kuwalea muda mwingi ili kujiepusha na
majanga kama haya.

Aidha
Mwanri aliwashukuru wananchi, Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wao
waliouonyesha na kupelekea kupatikana kwa watoto hao wakiwa na afya
njema.

Kwa
upande wa baba mzazi wa watoto hao ambaye ni mtumishi katika Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mashaka Juma baba alisema watoto wake walipotea
nmamo Desemba 28 mwaka uliopita.

Alisema
mtoto wake mmoja akiwa na miaka mitano na mwingine mwaka mmoja na nusu
walipotea wakati yeye na mkewe wakiwa wamekwenda sokoni kununua mahitaji
na waliporudi ndipo walipobaini hawapo nyumbani kwao.

Juma
alivishukuru vyombo vya habari na viongozo wa mikoa ya Mbeya na Tabora
pamoja na wananchi huku akisema bado hajaamini kama kweli watoto wake
wamepatikana tena wakiwa hai.

Mama
wa watoto hao,Zuhura Kaswa,alisema bado haamini na kwamba alipotaa
taarifa za watoto wake kupotea alikuwa akilia na kumuomba Mungu muda
wote.

Wakati
huo huo mtuhumiwa anayedaiwa kuwatorosha watoto wawili wa mkoani Mbeya
na kumtelekeza mtoto mmoja nyumbani kwa mtu eneo la Chechemi katika
Manispaa ya Tabora Hawa Ally anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

Afisa
Ustawi wa Jamii Mkoa wa Tabora Baraka Makona alisema kuwa mtuhumiwa
huyo alimuachia mtoto mkubwa mwenye umri wa miaka mitano kwa nyumba ya
mkazi wa Chemichemi kwa madai anaenda na mdogo ili kumtafutia matibabu
na kuahidi kurudi baadaye.

mtuhumiwa hakurudi siku hiyo mwishoni mwa mwaka jana,jambo lililomfanya
mwananchi aliyetelekezewa mtoto,kutoa taarifa Polisi kesho yake siku ya
mwaka mpya.

Baraka
aliongeza mtuhumiwa alienda na mdogo hadi Nzega na kumpeleka Hospitali
kutokana na kuugua na ndipo ilipogundulika sio mtoto wake na wasamaria
wema kutoa taarifa polisi na mtuhumiwa kukamatwa.

baada ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupata taarifa za kupotea kwa watoto
hao,walifuatilia na kugundua mtoto mkubwa katelekezwa Manispaa ya Tabora
na mdogo akipatikana Mjini Nzega.