Wazee wa manispaa ya bukoba washiriki halfa ya chakula iliyoandaliwa na mbunge neema lugangira

 


MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira akizungumza jambo kwa Wazee 38 waliowakilisha Kata zote 14 za Bukoba Manispaa kwa lengo la hafla fupi ya chakula cha mchana cha pamoja.


Wazee wakimsikiliza kwa umakini MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira

MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira kushoto akikagua chakula alichopakua Mzee King wa Manispaa ya Bukoba


Baadhi ya Wazee wakipata chakula cha mchana kwenye halfa hiyo iliyoandaliwa na MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira


MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira kushoto akiwa na Mama Muhazi wakifurahia jambo wakati wa halfa hiyo


MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira kulia akiteta jamabo na REV.Bishop Peter Claver Benjamini ambaye ni mwanzilishi wa NGOs inayoitwa Saidia Jamii ya Wazee Tanzania (SAWATA) na Saidia Jamii ya Wazee Kagera (SAJAWAKA) na ameshiriki katika uandishi wa Sera ya Taifa ya Wazee

MBUNGE
wa Viti Maalumu Tanzania Bara
kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira (Mb.) katikati wakiwa kwenye picha
ya pamoja na wazee hao mara baada ya kupata chakula wakifurahia jambo

MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara
kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira (Mb.) amekutana na Wazee 38 waliowakilisha
Kata zote 14 za  Bukoba Manispaa kwa lengo la hafla fupi ya chakula cha
mchana cha pamoja. 

Akizungumza wakati akiwakaribisha kwenye hafla hiyo fupi Mhe Neema alisema ameamua kukutana na  wazee
hao ambao walifarijika sana huku wakionyesha tabasamu kubwa kutokana na ukarimu ulioonyeshwa na mbunge huyo

Mbunge Neema aliwashukuru wazee
hao kwa namna ambavyo walivyomuunga mkono na kumpa ushirikiano mkubwa
katika cha Kampeni za Kisayansi na m mchango mkubwa uliopelekea
Chama Cha Mapinduzi kupata Ushindi wa Kishindo.

“Kwa
kweli niwashukuru sana kwa manufaa ya chama chetu na Taifa kwa ujumla 
kwa mchango wenu mkubwa na ninaamini ushirikiano huu utakuwa endelevu na
wenye tija kwa manufaa ya chama chetu”Alisema 

Aidha, Mbunge Neema alisema
angependa kutumia fursa hiyo pia kuwapa mrejesho kuhusiana na changamoto za
wazee walizowasilisha kwake Kipindi cha Kampeni. 

Wakati anawakaribisha kwenye
chakula, Mhe Neema Lugangira (Mb.) alitumia fursa hiyo kuwaelezea wazee umuhimu
wa Lishe Bora hivyo akawapitisha kwenye menu ya lunch na kila aina ya chakula
kina madini na vitamini gani ambazo wanazihitaji zaidi wazee.  

“Wazee wangu mnamahitaji maalumu ya
Lishe Bora hivyo tutashirikiana pamoja kuona namna bora ya kuhakikisha
mnaongeza ulaji wa mbogamboga na matunda” Alisema

 Wazee wote walimshukuru sana
Mhe Neema Lugangira (Mb) kwa kuwakumbuka na kuwafanya wajiskie wana thamani na
walimuomba aendelee na utaratibu aliouanzisha wa kukutana na wazee kuwapa
mrejesho wa wanayomtuma na walimshauri kuwa utaratibu huo ufanyike kwa ngazi ya
Kata ili aweze kufikia wazee wengi zaidi na kupata uelewa wa kina juu ya
mahitaji ya wazee. 

 

Katika
halfa hiyo Jumla ya Wazee 38 wa Bukoba Manispaa walishiriki ambao
walijumuisha wazee wawakilishi kutoka Kata zote 14 za Bukoba Manispaa 
na Vijiwe vya Kahawa vya Uswahili na Seneti