Waziri simbachawene, taasisi ya sokoine wakutana kutambulisha


Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George
Simbachawene amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi kutoka
Taasisi ya Kumbukumbu ya Sokoine waliofika ofisini kwake lwa lengo la
kuutambulisha Mradi kuimarisha mfumo wa kupanga bajeti na kuhuisha
masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi hiyo Fasal Issa alisema Mradi huo wenye thamani ya
sh. bilioni 2 utatekelezwa katika wilaya za Mpwapwa, Chamwino na Kondoa
mkoani Dodoma.

Alisema
kuwa lengo la mradi huo ni kujengea uwezo wilaya hizo katika kuboresha
uhimili wa mabadiliko ya tabianchi hususan katika sekta ya maji.