Waziri ummy asema serikali inaendelea na mchakato wa kuboresha sera mpya ya afya

::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
 
Na.Faustine Gimu Galafoni.Dodoma

Waziri
wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mhe. Ummy mwalimu
amesema serikali inaendelea na mchakato wa kuboresha sera mpya ya afya 
ili kuimarisha huduma  za afya nchini badala ya kuendelea na sera
iliyopo kwasasa ambayo imepitwa na wakati.

Waziri
Ummy amesema hayo  jana Nov.27,2019 jijini Dodoma wakati akifungua
Kongamano  la sita la   afya nchini  lijulikanalo  “TANZANIA HEALTH
SUMMIT “ambapo pamoja na mambo mengine ameendelea kusisitiza  dhamira
yake ya kuwasilisha bungeni muswaada utakao lazimisha kila mtanzania
kuwa na bima ya Afya.
Waziri
Ummy amesema Sera ya Afya ya Mwaka 2017 imejikita zaidi katika masuala
ya tiba na si kinga hivyo Sera Mpya ya mwaka 2019/2020 itajikita zaidi
katika Masuala ya kinga kwani kinga ni bora kuliko tiba.

Aidha
,Waziri Ummy amesema katika sera Mpya ya Afya ya Mwaka 2019/2020
itaangalia mktadha wa kuwafikia wananchi huduma ya Afya yaani Afya kwa
wote kwa kuangalia vigezo muhimu vya uhitaji  tofauti ya na sera ya
iliyopo ambapo inasema zahanati kila kijiji bila kuangalia mzigo wa
Magonjwa ama geografia ya eneo husika.

Kwa
upande wake Rais wa Kongamano la Afya nchini Tanzania, Dokta Omary
Chillo  amesema Lengo la kongamano hilo ni kujadili changamoto
mbalimbali zilizopo katika sekta ya afya na namna ya kukabiliana nazo
ili kuleta ufanisi zaidi katika utendaji kazi.

Kongamano
la sita la Afya Mwaka 2019 limeanza Nov.27 hadi  28,2019  huku
likiandaliwa na Taasisi  sita ambazo ni  Wizara ya Afya Tanzania,Wizara
ya Afya  Upande wa Zanzibar ,Ofisi ya Rais TAMISEMI ,Tume ya Huduma za
kijamii ya Kikristo,Baraza la Waislam Tanzania[BAKWATA]  na Tindwa
Medical Services   na kaulimbiu ni ufanisi na Matokeo katika utoaji wa
huduma za Afya.