Waziri wa viwanda na biashara ashiriki mkutano wa 37 wa dharura wa jumuiya ya afrika mashariki kwa mtandao.

 

Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (katikati), Naibu
Waziri wa Madini Mhe. Prof Shukran Manya (kulia) na Mkurugenzi
Mkurugenzi Idara ya Mtangamano wa Biashara ya wizara Bw. Ali Gugu
(kushoto) wakishiriki Mkutano wa 37 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri kwa
Sekta za Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ulifanyika kwa njia ya mtandao 23/04/2021, Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mtumba, Dodoma.



Baadhi
ya washiriki wa Mkutano wa 37 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri kwa
Sekta za Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ulifanyika kwa njia ya mtandao 23/04/2021, Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mtumba, Dodoma



Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (kulia) akisikiliza kwa
makini mjadala wakati wa Mkutano wa 37 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri
kwa Sekta za Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ulifanyika kwa njia ya mtandao 23/04/2021, Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mtumba, Dodoma.




Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Naibu Waziri wa Madini
Mhe. Prof Shukran Manya ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano
wa 37 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri kwa Sekta za Biashara, Viwanda,
Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia
ya mtandao tarehe 23 Aprili, 2021 katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.


Mkutano
huo wa 37 ulilenga kujadili uendelezaji wa Sekta ya Viwanda katika
Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuzingatia maelekezo yaliyopita ya Wakuu
wa Nchi na Baraza la Mawaziri la Jumuiya kupitia mikutano mbalimbali
iliyopita na kwa kuzingatia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la
Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Aidha,
Mkutano huo ulihudhuriwa na nchi zote sita (6) Wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, na
Sudani Kusini ulikuwa chini ya uenyekiti wa Jamhuri ya Kenya na Katibu
wa Mkutano huo alitoka nchi ya Burundi.


Ujumbe
wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof.
Kitila Mkumbo (Mb.), aliyeambatana na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Prof.
Shukurani Manya (Mb.) ulijumuisha Maafisa Waandamizi kutoka Wizara za
Viwanda na Biashara; Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Wizara ya Kilimo; Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo) na Wizara Madini.


Pia,
Mkutano huo wa 37 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara,
Viwanda, Fedha na Uwekezaji ulitanguliwa na mkutano ngazi ya Watendaji
Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika sekta hizo uliofanyika kwa
njia ya mtandao tarehe 22 Aprili, 2021 na ngazi ya Wataalam wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki Mahsusi katika eneo la Viwanda uliofanyika kwa njia
ya mtandao kuanzia tarehe 20 hadi 21 Aprili, 2021 katika Ukumbi wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, uliopo katika
Mji wa Magufuli Mtumba, Jijini Dodoma.


Ujumbe
wa Tanzania katika ngazi ya wataalamu katika mkutano huo uliongozwa
na Wizara ya Viwanda na Biashara na ulihudhuriwa na Wataalam kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya
Viwanda na Biashara, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Fedha na
Mipango, Wizara ya Madini, Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),
Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Kuhudumia Viwanda
Vidogo (SIDO), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Shirika la Utafiti
na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Chama cha wazalishaji nguo na bidhaa za nguo Tanzania (TEGAMAT) na Mfamasia Mkuu wa Serikali.