Mwakyembe: ni heshima kutembelewa na miss world

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Arusha
Ni
heshima kubwa kwa Tanzania kutembelewa na Mwenyekiti na Mwendeshaji wa
Shindano la Miss World Bi Julia Morley pamoja na Mshindi wa Miss World
2018 Vanessa Ponce.


Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.
Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa taulo za kike zinazojulikana
kama Uhurupads uliofanyika leo katika shule ya sekondari Moshono iliyopo
jijini Arusha.
“Ujio
wao leo hapa Arusha, ni heshima kwa taifa. Katika mataifa yote duniani,
wameichagua Tanzania, hii ni heshima kubwa na wametuletea zawadi ya
Uhurupads ambazo zitawaweka huru watoto wetu katika kutimiza ndoto zao
hasa wanapokuwa shuleni” amesema Waziri Dkt. Mwakyembe.

Aidha,
Waziri Dkt. Mwakyembe amesema kuwa bidhaa ya taulo hizo alizozindulia 
ni rafiki kwa mazingira kwa kuwa zinaweza kutunzwa mahali popote na
zisiwe na madhara kwenye mazingira kwa kuwa haina  mchanganyiko wowote
wa plastiki. Taulo hizo zinazotengenezwa na kikundi cha wanawake 12
kiachojulikana kama timu ya Uhuru Kit Ltd ambao wanaunga mkono juhudi za
Serikali katika kutunza mazingira kwa marufuku ya matumizi ya mifuko ya
plastiki nchini Julai, 2019.
Katika
kuhakikisha Tanzania inatumia vema fursa ya ujio wa Mshindi wa Miss
World 2018 Vanessa Ponce wa Mexico, Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Serikali
itaandaa ziara maalum kwa Uongozi wa Miss World ukiongozwa na
Mwenyekiti na Mwendeshaji wa Shindano la Miss World Bi Julia Morley
kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini ikiwemo mbuga za
Serengeti, hifadhi ya Ngorongoro pamoja na mji wa kihistoria wa
Zanzibar.
“Uwepo
wa Miss World 2018 Vanessa Ponce, dunia nzima macho yao yapo hapa
nchini, ni vema kuitangaza nchi yetu kimataifa kupitia ujio wake”
amesema Waziri Dkt. Mwakyembe.

Kwa
upande wake Mwenyekiti na Mwendeshaji wa Shindano la Miss World Bi
Julia Morley amesema kuwa amefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na
Serikali ya Tanzania ambapo ni mara ya kwanza kwake kuja nchini.
“Nimefurahi
sana Tanzania ni nchi nzuri, nilipopanda ndege kuja hapa nilipata
matangazo yanayosisitiza marufuku ya kutumia mifuko ya plastiki,
Serikali imefanya vizuri kujali kutunza mazingira” alisema Bi Julia
Morley.

Nao
Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico pamoja na Miss Tanzania
2019 Sylivia Sebastian wamesema kuwa urembo ni heshima, UhuruPads
zitawasaidia wasichana kupata elimu wakiwa huru wakizingatia kauli mbiu
ya ‘Uzuri wenye malengo.’ 
Uzinduzi
huo ulihudhuriwa na Mwenyekiti na Mwendeshaji wa shindano la Miss World
Bi Julia Morley, Mshindi wa Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka
Mexico, Mshindi wa Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian Bebastian Bebwa
pamoja, mwandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzania Bi. Basilla Mwanukuzi
pamoja na walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Moshono ya jijini
Arusha.