Watani wa jadi, Simba SC na Yanga
wamegawana pointi baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Kwa sare hiyo, Simba SC inafikisha
pointi 35 katika mchezo wa 14, hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa
pointi 10 zaidi ya mahasimu wao hao wa jadi, ambao hata hivyo wamecheza
mechi 12 tu.

Katika mchezo wa leo, mabingwa watetezi
Simba SC ndiyo walioanza kupata kupata bao mwishoni mwa kipindi cha
kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake wa kimataifa wa Rwanda, Meddie
Kagere.

Kagere alifunga bao hilo dakika ya 42
kwa penalti ya utata iliyotolewa na refa Jeonisia Rukyaa baada ya beki
wa Yanga, Kelvin Yondan kumvuta kwa mkono Mnyarwanda huyo nje kidogo ye
boksi, lakini akaenda kuangukia ndani.

Wachezaji wa Yanga SC walilalamikia
adhabu hiyo wakimuambia refa madhambi yalifanyika nje ya boksi, lakini
mwanamama huyo hakubadili uamuzi wake.

Dakika ya kwanza tu baada ya kuanza
kipindi cha pili Simba SC wakafanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa
kiungo Deogratius Kanda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
akimalizia pasi ya Kagere.

Kiungo mpya, Balama Mapinduzi akaifungia
Yanga SC bao la kwanza kwa shuti la umbali wa mita 30 baada ya
kumpokonya mpira kiungo wa wapinzani, Muzamil Yassin dakika ya 49.

Wakati Simba bado wanajiuliza, Yanga SC
wakafanikiwa kusawazisha bao la pili kupitia kwa kiungo wake, Mohamed
Issa ‘Banka’ dakika ya 53 akimalizia kwa kichwa krosi ya beki wa
kushoto, Adeyoum Ahmed.

Baada ya hapo, timu hizo ziliendelea
kushambuliana kwa zamu na kosa kosa za pande zote mbili, huku makipa wa
timu zote, Aishi Salum Manula wa Simba na Mkenya Farouk Shikhalo wa
Yanga wakifanya kazi nzuri.

Wafungaji wote wa mabao ya pili
hawakumaliza mchezo huo baada ya kuumia akianza Deo Kanda wa Simba SC
ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Hassan Dilunga dakika ya 52 na
Mohammed Issa wa Yanga aliyempisha Deus Kaseke dakika ya 69.

Wachezaji watatu walionyeshwa kadi za njano, mabeki Juma Abdul na Ally Mtoni ‘Sonso’ wa Yanga na Kagere wa Simba SC.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi
Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Tairone Santos,
Paschal Wawa, Jonas Mkude, Deo Kanda/Hassan Dilunga dk52, Muzamil
Yassin, Meddie Kagere/ John Bocco dk69, Clatous Chama na Francis Kahata.

Yanga SC; Farouk Shikhalo, Juma Abdul,
Adeyum Ahmed/ Andrew Vincent ‘Dante’dk64, Kelvin Yondan, Ally Mtoni
‘Sonso’, Abdulaziz Makame/ Yikpe Gislein dk62, Mohammed Issa ‘Banka’/
Deus Kaseke dk69, Mapinduzi Balama, Ditram Nchimbi, Papy Kabamba
Tshishimbi na Haruna Niyonzima.
Chanzo – Binzubeiry