Watanzania washindwa kutamba mashindano ya riadha ya vyama vya michezo a.mashariki(feasssa)

 Mathayo Sombi Mtanzania aliyeshika nafasi ya Pili katika mbio za mita 10,000 na kupewa medhali ya Fedha.
Mathayo Sombi Mtanzania aliyeshika nafasi ya Pili katika mbio za mita 10,000 na kupewa medhali ya Fedha.
Mathayo Sombi Mtanzania aliyeshika nafasi ya Piliakimalizia mbio kama anavyoonekana katika mbio za mita 10,000
Na.Vero Ignatus,Arusha.
Wanariadha
nchini wameshindwa kutamba katika katika mashindano ya riadha ya vyama
vya michezo kwa shule za Sekondari Afika Mashariki (FEASSSA)
yaliyofanyika Jijini Arusha.

Katika
Matokeo ya jumla kwa wanawake na wanaume nchi  Kenya iliongoza kwa 
kuondoka na jumla ya Medali 18 za Dhahabu, Medali 11 fedha na medali 10
za shaba na kufanya jumla ya medali  39 sawa na pointi 359.

Uganda
ilifuatia mshindi wa pili kwa kukusanya jumla ya Medali 10 za
dhahabu,Medali 14 za fedha  na 10 za Shaba na kufanya jumla ya Medali 34
walizonyakua ambazo ni sawa na pointi 334 huku Tanzania ikishika nafasi
ya tatu kwa kuambulia Medali 2 za dhahabu, Medali 5 za fedha na medali 8
za shaba ambazo ni sawa na pointi 209 .

Nchi ya Rwanda ilishika nafasi ya nne kwa kupata jumla ya medali 2 pekee za shaba na Zanzibar haikupata kitu.

Kwa
upande wa wanawake walioshoriki riadha mbio tofauti tofauti  Kenya
ilifanikiwa kunyakua jumla ya medali 7 za dhahabu, medali 5 za fedha,
medali 6 za shaba.

Nchi
ya Uganda ilifuata kwa wanariadha wake kufanya kweli  kwa kujikusanyia
jumla medali 6 za dhahabu,medali 8 za Fedha na medali 4 za shaba huku
wenyeji Tanzania wakiambilia medali 2 za fedha,2 za fedha na tano za
Shava, huku Zanzibar na Rwanda hazikupata kitu.

Kwa
upande wa wanaume Kenya ilijikusanyia jumla ya Medali 11 za Fedha, 6 za
fedha na 4 za Shaba , Uganda ilifuata kwa kuwa na jumla ya Medali 4 za
dhahabu,6 za fedha na 6 za  Shaba ,Tanzania haikupata kitu katika
dhahabu,ilipata medali 3 za fedha  na tatu za Shaba  huku Rwanda
ikiondoka na medali 2 za Shaba na Zanzibar haikuambulia kitu.
Matokeo
mengine mwanariadha Faith Kipsang  kutoka Shule ya St. francis ya
Kenya  alichaguliwa kuwa mwanariadha Bora kwa wanawake huku mwanariadha
Layeng Eric Sibryanda kutoka Gombe  nchini Uganda aliibuka mwanariadha
bora kwa wanaume.

Kocha
wa timu ya Riadha ya Tanzania katika michuano ya FEASSSA Robert Kalyahe
alisema ni kweli wanariadha kutoka Kenya wamefanya vizuri kwa kuondoka
na medali za kutosha na Tanzania kupata vichache 
” Tumepigwa
kwani pia tumeokoteza tu vijana kutoka mashindano ya  Umiseta
yaliyofanyika Mtwara na muda wa mafunzo ulikuwa mfupi,hali ya hewa pia
ilituchanganya hapa Arusha lakini yote kwa yote tumejifunza kutoka kwa
wenzetu Kenya na tutajua nini cha kufanya,”alisema Kalyahe.

Alisema
Tanzania inapokosea ni kuweka muda mchache inatakiwa kuweka muda mrefu
wa maandalizi vijana wachaguliwe mapema tena ikiwezekana wachezaji
wawekwe katika shule moja ili kuwa na maandlaizi ya kutosha.

Naye kocha wa riadha na mjumbe wa kamati
tendaji ya Riadha Tanzania Yohana Misese alisema katika riadha
inasikitisha kwani watanzania wamekuwa wakienda kwenye mashindano na
kurudi bila kufanya tathmini wapi wanakosea .

Tumeona
wenzetu wako makini katika maandalizi na timu wameandaa kwa muda mrefu
tofauti na sisi tumeandaa kwa wiki mbili hali inayopelekea kuwa na
maandalizi yasiyo na Matokeo mazuri,” alisema Misese.