WASIRA ATAMBA BADO ANA UWEZO KUSHINDA UBUNGE

MKONGWE  wa  siasa nchini Tanzania mbunge aliyekuwa ameondolewa madarakani na CHADEMA Steven Wasira  ametangaza nia ya kuutaka
tena Ubunge wa Bunda Mkoani Mara kwa ticket ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
ambapo baada ya kutangaza nia baadhi ya Watu wameanza kumkosoa kwamba
ana umri mkubwa hivyo anatakiwa kupumzika.

Wasira ambaye ana umri wa miaka 75 sasa
hivi amesema “uwezo wa kuendelea kuwahudumia Wananchi wa Bunda kama
wakinipa ridhaa upo ndio maana nimeamua kurudi na kuchukua fomu ya
kuomba ridhaa”

“Kitu ambacho wengi wanakosea, Bunge ni
kioo cha Jamii na ndio kinachowakilisha Watu wa Tanzania na Watu wa
Tanzania wana marika yao, kuna Vijana, Wanawake, Wazee, Walemavu n.k
kwahiyo Katiba haikusema ukifika umri flani huwezi kugombea”

“Na kwenye kugombea sipo peke yangu…
wako Wazee wengi wanagombea mi sijui kwanini naulizwa mimi tu
hahahahha…. Mzee Andrew Chege tunalingana umri na yeye anagombea kwanini
wana-react upande wangu tu?”

“Hata hivyo kukosolewa hakunitoi mimi
kwenye mstari, mimi nasoma maoni yote yanayoniunga mkono na yasiyoniunga
mkono, wawaache wapiga kura wa Bunda waamue, kwanza stage tuliyonayo ni
ya ndani ya Chama, tungoje kwanza Wanachama wa CCM kupitia Mkutano Mkuu
wa Jimbo watatoa maoni yao”

“Kama wanafikiri hawahitaji Kiongozi
mwenye umri wangu si wataninyima kura bwana……. lakini ukiona wamenipigia
basi maana yake wanahitaji busara zangu na ushawishi wangu kwa ajili ya
maendeleo yao, kwahiyo mimi sioni hoja ya reaction… sasa sijui reaction
inatoka CCM au Upinzani… sielewi”

Chanzo ;millardayo.com